Ukifika wakati wa kuachana sio lazima mgombane

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
505
Reaction score
872
Kuna wakati itabidi uachane na mbia wako (Business Partner) wa biashara ambaye mlipanga kufika mbali sana. Kuna wakati itabidi uachane na bosi wako ambaye ndiye alikusaidia kukufundisha kazi hapo mwanzo.

Kuna wakati itabidi uachane na mtu uliyekuwa unampenda sana na ulidhani utakuwa naye kwa muda mreeefu. Kuna wakati katika maisha utalazimika kuachana na watu, ofisi.... n.k. Ukifika wakati huu kuna mambo ya kuzingatia.

Moja, sio lazima UANZISHE UGOMVI na unaoachana nao. Unaweza kuachana kwa HESHIMA na UTULIVU. Kumbuka kuachana sio VITA, mnaweza kuachana na maisha yakaendelea. Sio lazima uwageuze ADUI wale unaowaacha au wanaokuacha.

Maisha yana majira na kila mtu anatakiwa kuwa mahali fulani kwenye majira tofauti. Mbili, pokea maumivu na yakubali. Haitasaidia kutokubali uhalisia. Kama mtu ameamua kuondoka, hakuna namna. Haitasaidia kukataa uhalisia, badala yake jipange kwa hatua inayofuata.

Tatu, usijilazimishe kuonyesha ubaya wa unayeachana naye. Kumbuka mafanikio ya UNAKOKWENDA hayajabebwa na watu kujua ubaya wa UNAYEACHANA naye bali yamebebwa katika DHAMIRA SAFI ya UNACHOKWENDA KUFANYA.

Hakuna umuhimu wa kumpaka matope unayeachana naye.
 
Kuna watu tunapenda kuachana kwa amani, Ila upande mwingine hauoni Hilo.
Mfano kumdai mtu, wewe unaweza usiwe na nia ya ugomvi Ila mdaiwa akapelekea mgombane mpaka mvunje urafiki.
 
Karushe mawe juu ya bati lake mwaga mchanga dirishani.....😁
Shonashona mdoli funga pamoja na kinyonga weka mlangoni Kwake likiamka asubuhi likifungua mlango tu lishtuke,heart attack,lidondoke,lizimie liibukie hospital likizinduka lishtukie Lina pop ya kichwa lilivyodondoka lilidondokea uchogo ukaburst.Mama.e.😠😏
 
Huku ndio kuachana sasa, yani unaachana unasalimiana ndio nini.....🤣🤣🤣
 
Shonashona mdoli funga pamoja na kinyonga weka mlangoni Kwake likiamka asubuhi likifungua mlango tu lishtuke,heart attack,lidondoke,lizimie liibukie hospital likizinduka lishtukie Lina pop ya kichwa lilivyodondoka lilidondokea uchogo ukaburst.Mama.e.😠😏
Aisee siku nitakayo kupiga kibuti....itabidi tugawane majengo ya serikali...ima wewe uende polisi au Mimi niende hospitali au vice versa maana si Kwa maneno hayo honey!
 
Afu huwa naandika tu ❤️ mi nikiachana na mtu nakubali kuwa so wangu tena naondoka sigeuzi shingo tena forever.Maisha mengine yanaendelea😉
 
Kuna wakati itabidi uachane na mbia wako (Business Partner) wa biashara ambaye mlipanga kufika mbali sana. Kuna wakati itabidi uachane na bosi wako ambaye ndiye alikusaidia kukufundisha kazi hapo mwanzo.

Kuna wakati itabidi uachane na mtu uliyekuwa unampenda sana na ulidhani utakuwa naye kwa muda mreeefu. Kuna wakati katika maisha utalazimika kuachana na watu, ofisi.... n.k. Ukifika wakati huu kuna mambo ya kuzingatia.

Moja, sio lazima UANZISHE UGOMVI na unaoachana nao. Unaweza kuachana kwa HESHIMA na UTULIVU. Kumbuka kuachana sio VITA, mnaweza kuachana na maisha yakaendelea. Sio lazima uwageuze ADUI wale unaowaacha au wanaokuacha.

Maisha yana majira na kila mtu anatakiwa kuwa mahali fulani kwenye majira tofauti. Mbili, pokea maumivu na yakubali. Haitasaidia kutokubali uhalisia. Kama mtu ameamua kuondoka, hakuna namna. Haitasaidia kukataa uhalisia, badala yake jipange kwa hatua inayofuata.

Tatu, usijilazimishe kuonyesha ubaya wa unayeachana naye. Kumbuka mafanikio ya UNAKOKWENDA hayajabebwa na watu kujua ubaya wa UNAYEACHANA naye bali yamebebwa katika DHAMIRA SAFI ya UNACHOKWENDA KUFANYA.

Hakuna umuhimu wa kumpaka matope unayeachana naye.

Kila mtu ashinde mechi zake
 
Afu huwa naandika tu ❤️ mi nikiachana na mtu nakubali kuwa so wangu tena naondoka sigeuzi shingo tena forever.Maisha mengine yanaendelea😉
Safi Sana❤️.....upo kama mm honey! Huwa sina Mda wa kulialia coz mambo mengi na Mda wenyewe mchache hapa duniani
 
Back
Top Bottom