Ukifuga hata ng'ombe mmoja tu wa maziwa, mwajiriwa hakufikii

KUMBUKIZI 📌

Hapa tulipata fursa ya kumtembelea Mzee Hassan Migeto, mfugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka Mkuyuni – Mwanza.
Alitueleza kwa uwazi safari yake ya ufugaji, changamoto alizokumbana nazo mwanzoni—ikiwemo kukosa ng’ombe bora na uhaba wa malisho ya uhakika.

Kupitia kujifunza, kufanya marekebisho sahihi, na kusimamia ufugaji wake kitaalamu, leo Mzee Hassan anafanya vizuri. Mapato ya ufugaji wake yameweza kumuwezesha kujenga nyumba yake na kuboresha maisha kwa ujumla.

Kwa kauli yake mwenyewe anasema: “Ukipanga na kufuga kitaalamu, hata mfugaji mwenye ng’ombe mmoja anaweza kupata kipato ambacho mwajiriwa wengi hawakifikii.”
View attachment 3527868
Kwani wewe mfuga cow hauwezi kuwa na mafanikio yako bila kujifananisha na mwajiriwa?
Ebu achaneni na huu ujinga wa kupenda kufananisha kila kitu.
 
Embu twende kwa namba, ngombe anatoa lita 30 kwa siku, kama lita ni bku jero kwa day unapata 45k, ukitoa 25k ya kumuhudumia unabaki na 20k ambayo kwa mwez ni 600k, hujamzidi mwajiriwa ktk sekta fulani, niamua kuwa motiveshen supika na mm.
Hao ng'ombe wa huyo dingi wakitoa sana ni lita 5 tu. Wamekonda kinyama.
 
Ng'ombe wa maziwa hauzwi laki 4 ni kuanzia mil 4 kwa ng'ombe mmoja

Ng'ombe wa kutoa lt 10 huyo sio ng'ombe, ng'ombe wa maziwa anatakiwa kutoa angalau lt 15 .
Mimi ninao watatu 3 aina ya Ayrshire, wanatoa lt 48 kwa siku, nauza Lt 45.
45×1600=72,000 kwa siku
30×72,000= 2,160,000/-
Ili uuze Lita kwa 1600 inabidi uwe unaishi mjini kidogo ambapo malisho hamna. Imagine Mbeya ni jiji ila Lita ya maziwa mfugaji anaiuza kwa shilingi 1,200.

Ukikaa sehemu isiyo na malisho gharama za uendeshaji ni kubwa. Unahitaji gari dogo kama Suzuki Carry au pikipiki ya gurudumu tatu ya kubinua ili ulete majani au pumba, au ukodishe.

Ukichanganya na eneo la kufuga kama mjini lina thamani kubwa. Ng'ombe wenyewe hao watatu ni milioni 13 jumla.

Sasa mtu anayeropoka tu kwamba mwajiriwa anashindwa kipato na mfugaji anachukulia kwamba kufuga ni kama matako tu kila mtu anayo kwahiyo asiyefuga basi hataki. Mtu yeyote anayefuga kisasa ana uwezo wa kuwa mmiliki wa duka, au bajaj kadhaa au bodaboda kadhaa za mkataba, au biashara nyingine. Hivyo vyote vinataka mtaji sio kuwa na ajira au kuwa jobless. Yeyote aliyepata mtaji kwa kurithi, kukopa, kudunduliza mshahara, kupewa or any means na akawa na nia ndio anaweza.
 
Nakumbuka kauli Maalumu ya Proffesor mmoja "It is cheap to keep a wife, Than keeping one dairy Cow"

Kweli, Ufugaji wa Ng'ombe sio Matrako kwamba kila mtu lazima awe nayo, Wengine tubaki kufuga broiller 3miln na kapagala kamoja tu unaishi.
 
Yaani kufuga ng'ombe mmoja wa maziwa unakuwa na maisha mazuri kuliko CEO wa vodacom?

Mijitu miongo ka tume ya mo29 khaaaaa!
Walitakiwa tuu kusema Inakupa stable income ila sio kuwa zaidi ya mwajiri hata wa Masijala.

Kumbuka risk kwenye Kilimo is very high ukikinganisha na Ajira.
 
KUMBUKIZI 📌

Hapa tulipata fursa ya kumtembelea Mzee Hassan Migeto, mfugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka Mkuyuni – Mwanza.
Alitueleza kwa uwazi safari yake ya ufugaji, changamoto alizokumbana nazo mwanzoni—ikiwemo kukosa ng’ombe bora na uhaba wa malisho ya uhakika.

Kupitia kujifunza, kufanya marekebisho sahihi, na kusimamia ufugaji wake kitaalamu, leo Mzee Hassan anafanya vizuri. Mapato ya ufugaji wake yameweza kumuwezesha kujenga nyumba yake na kuboresha maisha kwa ujumla.

Kwa kauli yake mwenyewe anasema: “Ukipanga na kufuga kitaalamu, hata mfugaji mwenye ng’ombe mmoja anaweza kupata kipato ambacho mwajiriwa wengi hawakifikii.”
View attachment 3527868
Kwa idadi ya ng'ombe kuanzia 5 ni sawa anazidi Watumishi wengi zaidi wa kada za chini.
 
Ufugaji unalipa sana na wenzetu wakenya wameuchukulia serious sana, mtu mwenye ng'ombe 2 bora wa maziwa anaishi vizuri sana kuliko hata mwajiriwa.
Sasa hivi bei ya maziwa imepanda sana na mahitaji ni makubwa na ukiwa na ng'ombe husumbuki hata kutafuta wateja wa maziwa.
Binafsi sehemu nilipo hakuna mfugaji anakosa soko la Maziwa ila bei sio kubwa maximum ni buku but on average ni 700-1000/Lita.

Ukiwa na malisho Yako ya kupandwa na kausafiri ka kuhudumia shamba Inakupa hela.
 
Inategemea na muajiriwa gani Kuna watu wanavuta pesa ndefu
 
Back
Top Bottom