Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MKIGOMBANA NA MKEO, AKAENDA KWAO, USIMFUATE WALA USIMTAFUTE

Anaandika Robert Heriel.

Leo sina mengi ya kusema ndugu yenu. Nimefanya uchunguzi Kama mnavyonifahamu. Nikisemacho ni kweli tupu. Wala sisemi haya Kwa maslahi yangu, au ya mtu yeyote Yule. Nazungumza mambo ambayo ni kweli kabisa.

Na ujumbe huu usomwe na wangu wote. Mnisikie na kuyafuata ninayoyasema, Kwa maana maneno yangu yamepimwa na kuthibitika kuwa hayana madhara kwenu.

Kabla hujaoa jifunze kuwa Mwanaume. Niliwahi sema, mwanaume ni AKILI.
Kabla hujawa Baba jifunze kuwa Mtawala.
Na ili uwe Mtawala yakupasa uwe na hekima na busara. Pia uwe na maamuzi yasiyo yumba(uwe na msimamo).

Kitu kikubwa Kwa Baba ni Heshima, mwanaume Bora hulinda heshima yake kuliko kitu chochote. Yupo tayari kupoteza vyote lakini sio kupoteza heshima yake Kama Baba. Ndio maana Baba bora ni rahisi kufukuza mke na watoto pale anapoona heshima yake IPO hatarini.
Mwanaume anayepuuza heshima yake na kujali vitu vingine anapoteza sifa ya kuitwa Baba.

Mwanaume aliyeiva kamwe hawezi sumbuliwa na Mwanamke. Mwanaume ili asumbuliwe na mwanamke na hapa nazungumzia mke wake sharti aongozwe zaidi na Hisia pasipo Akili. Na siku zote mwanaume anayeongozwa na Hisia huyo sio mwanaume halisi.
Kama nilivyosema hapo juu. Mwanaume ni AKILI. Sio ajabu kwenye maandiko waliposema ishini na wake Kwa Akili.
Tafsiri yake ni kuwa pasipo akili heshima ya mwanaume ipo mashakani.

Baba ni jina kubwa. Baba hakosei. Na hapa namaanisha Baba aliyejifunza kuwa Mtawala.
Ikiwa Baba hakosei, tafsiri yake Baba haombi Msamaha.

Baba kuomba msamaha tafsiri yake hajielewi, hakujua alichokuwa anakifanya, Baba sharti awe na msimamo hata Kama wengine watamuona anakosea. Huyo ni Baba. Baba hapaswi kuwa kigeugeu.

Tuna Baba wawili, Baba WA kweli, ndiye MUNGU muumba wa mbingu na Nchi. Na yupo Baba wa uongo ndiye Ibilisi.
Ibilisi Kama Baba mpaka Leo anaamini yupo sahihi, licha ya wengi kuona alikosea. Ubaba ndio upo hivyo. Unapaswa uwe na msimamo. Ikiwa Baba unapaswa kuwa na msimamo basi yakubidi kabla yakufanya maamuzi yoyote lazima utumie akili ili ufanye uchaguzi uliosahihi kwako.

Ikiwa mwanamke ambaye ataitwa/utamuita Mkeo mkakosana, iwe Kwa sababu yoyote Ile, iwe wewe ndiye chanzo cha ugomvi au yeye ndiye chanzo cha ugomvi. Akaondoka kukimbia kwenda kwao pasipo wewe kumfukuza,
Akaenda kwao wakamlaki Kwa sababu ni mtoto wao, wakijua walimuozesha kwako,lakini wakampokea,
Kamwe usijeenda kumchukua, wala USIMTAFUTE, wala usitake Suluhu naye.

Utamhesabia siku saba za mwanzo, ikiwa hajakutafuta, utamhesabia siku Saba zingine, ikiwa hatajishusha, mhesabie siku saba zingine mpaka zifike siku 28, asipokuja achana naye kabisa wala usihesabu tena siku.


Ikiwa atarudi kabla hata ya mwezi Kuisha utampokea, kisha utampa barua awapelekee wazazi wake, waandikie na Fidia kadiri utakavyoona kulingana na siku alizokaa, na utoe onyo kuwa kama tabia hii itajitokeza wakati mwingine, barua hiyo itahesabika Kama sehemu ya onyo la mwisho, hivyo akirudi basi mtoto wao utampa talaka.
Ikiwa watashindwa kulipa fidia waambie asirudi wakae naye, au wanaweza kumuozesha na barua hiyo itahesabika Kama talaka kwani sababu utakuwa umeziorodhesha.

Mwanamke kuondoka nyumbani pasipo iidhini ya Mumewe ni kosa tosha la kumfukuzisha kwenye nyumba yako, isipokuwa Kwa sababu zinazohatarisha usalama wake kama kupigwa na mumewe ikiwa ni Wale wanaume vichwa maji. Na hapa kupigwa namaanisha kupigwa haswa sio Yale makofi mawili matatu ya kuonywa.

Mwanamke anapokimbilia kwao na akapokelewa na wewe ukaenda kumchukua ni dalili kuwa utawala wako umepinduliwa na sasa wewe mama Mtawala hauko utawalani.
Mwanamke kama itatokea akaona sababu ya kukimbia nyumbani kwako basi itampasa akimbilie kwenu, yaani Kwa Mama yako au Baba yako(akimbilie ukweni).
Hiyo ndio Heshima.

Na ndio maana ya wewe kuoa na kumuita huyo ni Mkeo. Lakini sio jitu umelioa likufanyie mapinduzi, ati uende ukalichukue kwao, hiyo kamwe haiwezi fanywa na Mwanaume aliyefunzwa akawa Mtawala Kama ilivyosilika ya mwanaume.

Mwanaume haweziitwa kikao ukweni akaenda, isipokuwa ukweni wanauwezo wa kuwasiliana na Familia ya Mkwe wao(mwanaume aliyeoa binti Yao), kisha wazazi wa mwanaume waitishe kikao, kisha upande wa kiukeni ualikwe Kama wageni na watoe malalamiko Yao.

Ikiwa utakiuka na kukaidi maneno haya basi utajikuta katika taabu ambayo hukupaswa uipitie.

Wanawake wengi ukienda kuwachukua kwao, hugeuka Mateso kwako hapo baadaye, huwa wajeuri, lazima wakupelekeshe kwani wanajua kabisa kuwa huwezi ishi pasipo wao.
Nimeshuhudia haya Kwa sehemu kubwa, nimejionea Kwa macho yangu na kuyafanyia tathmini hivyo maneno yangu yamepimwa yakathibitika.

Jifunze kukaza roho kabla ya kuitwa Baba. Jifunze kufanya maamuzi magumu kabla ya kuitwa Mume. Baba ni Cheo ambacho anastahili mtu mwenye maamuzi magumu. Ubaba Kwa sehemu hauhitaji kuwa na huruma hata kidogo.

Mwanamke akienda kwao Kama hamna hata mtoto mmoja mwambie akae huko huko asirudi. Kama mtakuwa na walau mtoto mmoja kuendelea unaweza mfanyia subra Kama nilivyoeleza hapo juu ya siku 28 yaani kabla mwezi mwingine haujaandama awe karudi, Kama hajarudi fukuza. Wala usimsikilize yeyote.

Baba hasikilizi yeyote isipokuwa akili yake na namna ya kulinda heshima yake. Hakuna cha serikali, hakuna cha mchungaji sijui Sheikhe, hakuna cha wazazi. Linapokuja suala la heshima yako kama Mwanaume usimsikilize yeyote Yule.

Usiponisikiliza;
Kila siku utaenda kujidhalilisha ukweni kuomba omba misamaha Kama Juha,
Kujiliza Liza Kama Paka ukweni ati kisa mwanamke asiyejielewa.
Mwanamke akijua kuwa akikimbia kwao utamfuta atakuwa hata kitu kidogo kakimbia kwao, sijui nini kwao,

Usihudhurie vikao ambavyo havina msingi wowote.
Mpaka wanakuozesha binti Yao waliridhishwa na kuwa wewe ndiye utakayemsimamia na kumhudumia mtoto wao.

Nafahamu kuna watu watanipinga, Hilo sitalijali na ninalitarajia.
Kuna watu watasema kuwa ninadada au nitazaa watoto wakike, Ndio ni kweli; mashemeji zangu na wakwe zangu WA baadaye utaratibu ni huo nilioutoa.

Kama nitakupa binti yangu akaleta upuuzi wa kukukimbia, Kwanza sitampokea, lakini kama atapata njia mbadala ya kwenda Kwa watu wengine. Fukuza na nitakupongeza na kukuona wewe ulistahili kumuoa mwanangu.

Lakini binti nimekupa alafu kakukimbia alafu unaleta pua yako kwangu, hakika nitakutoa nduki na panga mchana kweupe.

Be a Man not like a man.

Nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Nakazia.
Kama umeongelea kabisa kisa cha jamaa angu mmoja,
Yy alikuw anamfata mkewe kwa mamamdogo wake alipokuw anakimbilia,
Akifika huko anajiliza kibwebwege mke anarudi,
Sasa hivi ni kama mke kamuacha kbs.
 
Mke wangu hawezi kuacha nyumba nzuri hivi aliyoipambania kuipendezesha miaka mingi yenye kila kitu akaenda kwao, labda wewe ndo umwache hapo uende kwenye nyumba nyingine. Utamuulia hapo ndani ila HATOKI😂


Na Mwanaume mwenye akili hawezi mfukuza mke wake pasipo sababu ya msingi nayo ni kuondolewa heshima yake.

Ikibidi kuuawa atauawa
 
Back
Top Bottom