Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Yeah kwa kizazi hiki cha 90’s kuja 2K’s kundi kubwa la vijana ni goigoi tu na wanawake wengi ndio wameinuka kiuchumi kupitia fursa mbalimbali na sera za kuwapa kipaumbele.🤣🤣🤣🤣🤣
Na wengi wapo kundi hili
Its hard kwa kweli, vijana wachache ndio wamefanikiwa kuishi katika misingi ya kiume wakiwa na finacial muscles na kukabili majukumu yao kwa uhakika. Hapa kuna walioajiriwa na wenye vipaji hasa vya usimamizi wa biashara.
Sasa imagine hali iliopo sasa wanawake wengi wanajikuta wanalea wapenzi wao sio kwa kupenda ila unakuta mwanamke kutusua ni easy akitia tia huruma kapewa mtaji au kama amesoma kapewa shavu!
Kwa mwanaume ajira ni ngumu kupata gombania goli sana inabidi wa capitalize kwenye hustling na ku hustle sio kitu ya kila mtu aisee! Business is for people with talent & passion. Vijana wengi wamekuwa raised kwenye mfumo wa kuajiriwa kuingizwa kwenye payroll tu! Hali ikiwa tofauti wanachanganyikiwa yani ndio wengi wanaishia kubeti tu mtaani😄 na kuishia kutafta mbeleko kwa mademu zao!
Mtu wa aina hii ni ngumu kuweka misimamo ya namna hio mbele ya mwanamke! Kuna dada yangu mmoja aliniambia “ukikosa pesa unakosa power ya kufanya decision”. You can not stand on what you believe kama unategemea support ya mtu au watu flani kujiendesha!