Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Ukigombana na Mkeo, akaenda kwao; USIENDE wala Usimtafute

Wanawake ni noma tizama mibaba inavyojiliza kama mitoto, kujadiliana tu humu imeondoa uanaume wenu maana yake mnatuogopa😅😅😅 walio wanaume hawana hizi kelele Ni vitendo tu, pumbavu zenu
 
Wanawake ni noma tizama mibaba inavyojiliza kama mitoto, kujadiliana tu humu imeondoa uanaume wenu maana yake mnatuogopa😅😅😅 walio wanaume hawana hizi kelele Ni vitendo tu, pumbavu zenu

Kama ndivyo unavyofikiri ni Sawa kwako,
 
Unawadaganya wenzako na sidhani ka umeoa hapo ulipo. Ubabe wa kijinga haujawahigi kuwa na tija sometimes kujishusha sio udhaifu
Anachokiongea ni kweli, ni salama kwa familia yenye misingi na maadili ya kiafrika..
Mwanume hutakiwi kuyumba katika maamuzi.
 
Ninae bro wangu mmoja namkubali sana jamaa Yuko real mbaya alaf Hana maneno mengi Yani.

Sasa wife wake alizingua yani mke ndo alikua chanzo Cha maneno siku hiyo kaenda kazini mke akaamua kumtumia jamaa sms kumwambia kuwa anataka kuondoka arudi kwao kwahyo amwambie sehem atakayo acha ufungo wa nyumba ili yeye aende kwao.

Mwamba akamuelekeza mwanamke sehem ya kuacha funguo, kweli bana jamaa jion karud nyumban kwake hakumkuta mke jamaa akavunga akatulia kimya, kesho yake akapiga simu kwao na mke kuuliza kama ameshafika, mama mkwe akaanza kumuwakia jamaa bila kuuliza chanzo, alafu mama mkwe akamwambia jamaa kuwa haya mambo hayawezi kumalizwa kwenye simu hivyo basi aende ukweni ndo watayaongea hivihivi haliishi na mke hawez kurud kwa jamaa.

Jamaa alicho jibu ni kuwa, Mimi sijamfukuza na chanzo Cha ugomvi ni mtoto wako mwenyewe, kwahiyo Mimi sina muda wa kuja huko kwaajili ya hili jambo, hivyo ni maamuzi yenu tu kuendelea kubaki nae Mimi kilicho nifanya nipige simu ni kutaka kujua tu kama kweli amefika nyumban kwakua umenithibitishia uko nae basi Mimi sina tatzo nipo na amani kwakua hamtaniliza chochote kwakua tayar mpo na mtoto wenu.

Siku zikaenda walivyoona jamaa Yuko kimya wao wenyewe wakampigia simu kumuomba msamaha mke akarudi nyumban mwenyewe na Hadi leo wanamuheshimu jamaa ile mbaya na adabu imeboreshwa kwa hali ya juu, ila mwamba angeenda kutembelea magoti ukweni Hadi leo ingekua migogoro haiishii.
 
Kila kitu ni ‘timing’ kuna muda wa kusimamia nafasi yako kama mwanaume na pia ku balance nafasi ya mwenzio/mkeo

Ukijifanya ubabe muda wote hautakaa na mwanamke nakuambia, unatakiwa kujua mipaka ya power yako na kiwango cha kutumia

Pia jua familia sio zote zinakubali mtoto wao akigombana na mwenzake arudi kwao sema tu inakuwa hakuna jinsi ya kumfukuza na hasa wakijua kosa ni la mtoto wao na unaweza kuta una watetezi kutoka huko huko familia ya mkeo maana wanamjua mtu wao labda tu na wewe uwe kimeo hasa

Nipo kwenye ndoa karibia miongo 2 , mleta uzi naomba pia uzoefu wako una miaka mingapi ktk ndoa? Labda tuanzie hapo kwanza
 
Unawadaganya wenzako na sidhani ka umeoa hapo ulipo. Ubabe wa kijinga haujawahigi kuwa na tija sometimes kujishusha sio udhaifu
Hajadanganya,amesema ukweli.Ndoa yangu ina miaka 15.Mwanzoni kabisa mwa ndoa nilimwambia mke kuwa katika vitu ambavyo asitarajie Mimi kufanya ni kuhudhuria kikao cha usuluhishi ukweni na kumfata kwa lengo la kumrudisha nyumbani iwapo ataenda kwao.Sijawahi kufanya hayo na imenisaidia sana.
 
Uzi Safi kabisa kwa wanaume tu.
Kuna mmoja alileta ufara na dharau Tena kwenye nyumba ya Kupanga sikutaka maneno Mengi Nilifanya maamuzi magum na sijawahi kujutia saa hvi anaisoma namba.
 
Hajadanganya,amesema ukweli.Ndoa yangu ina miaka 15.Mwanzoni kabisa mwa ndoa nilimwambia mke kuwa katika vitu ambavyo asitarajie Mimi kufanya ni kuhudhuria kikao cha usuluhishi ukweni na kumfata kwa lengo la kumrudisha nyumbani iwapo ataenda kwao.Sijawahi kufanya hayo na imenisaidia sana.
Hahaa Hilo Jina lako nawafaham watu design yako.
 
Hahaa Hilo Jina lako nawafaham watu design yako.
Yaani hii ni copy and paste kutoka kwa baba yangu.Enzi zile maza akizinguana na mshua ,maza anasepa kwao.Mshua anachuna.Tukimuuliza baba mbona mama harudi?Anasema wanangu nyie ni watoto wa kiume,kamwe usimfate mkeo kwao mkigombana.Mwacheni atarudi.

Kweli baada ya wiki moja,mbili maza anarudi,maisha yanaendelea.Bahati nzuri kwangu Mimi nilimwambia mke wangu mapema kabisa juu ya msimamo huo.

Tunazinguana lakini sijawahi kushitakiwa ukweni.Siku moja katika mazungumzo na baba mkwe akaniambia anaamini ninakaa na mtoto wake vizuri maana hajawahi kupata mashtaka yoyote.
 
Back
Top Bottom