Ukiijua kweli hutoteseka kamwe

Ukiijua kweli hutoteseka kamwe

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
915
Reaction score
1,082
Kuna watu hawaendi Msikitini wala kanisani, ila wako na Imani kubwa mno wako na matendo mema wanasaidia maskini wako na adabu wanamuheshimu kila mtu wenye dini zao na watu tofauti.

Unajilipua... unategemea upate pepo ya Muumbaji inakuingia akilini kweli? Waliotetea waafrika hawapo kwenye vitabu vya dini ila waliotetea dini ndo waliowekwa kwenye vitabu vyao. Uislamu umekuja kwa mijeledi watu wanajichwa wakikata kujiunga na hizi dini daah.

Leo hii Waafrika wengi wamejiunga na dini za Ukristo na Uislamu zinazomtangaza Mungu mmoja. Imani hizo zilikuwepo tangu miaka mingi katika sehemu kadhaa za Afrika lakini katika maeneo mengine Ukristo na Uislamu zilienea tu vizazi vichache vilivyopita zikiendelea hadi leo.

Dini za asili, Ukristo na Uislamu zinaathiriana katika Afrika. Hivyo kuna watu ambao wanafuata imani za jadi au walau sehemu za imani hizo. Kwa hiyo inafaa kupata picha ya imani katika jamii za Waafrika jinsi zilivyokuwa kabla ya kuguswa na Uislamu na Ukristo.

Dini za Kiafrika zinafuata imani maalumu, sawa kabisa na hizo za nje ambazo zimeleta mfumo mpya wa kuabudu. Badala ya kuabudia mapangoni au misituni kama Waafrika walio wengi walivyofanya kwa karne nyingi, zimehimiza kujenga makanisa na misikiti kwa ajili ya kumwabudu Mungu kadiri ya ufunuo wake mwenyewe.

Madhehebu mengi ya Kikristo yamekuwa yakimuabudu Mungu kwa kushirikiana na wafu wanaoheshimiwa kama watakatifu, wakati Waafrika tangu zamani waliwaenzi wazee wao waliokufa na kuwaita mizimu. Waafrika hao tangu zamani waliwaheshimu wafu kwenye makaburi yao, lakini baadhi ya Wakristo waliwaheshimu wafu kanisani kwa sala zao pamoja na kusujudu pengine masalia au picha za hao wafu.

🌹Katika Amri Kumi za Biblia, Waafrika kwa jumla walikuwa nazo hata kabla ya kuja kwa Wazungu: walijua kwamba imewapasa kuwaheshimu wazazi wao, kutoua, kutoiba wala kufanya kinyume na maagizo ya wazee wao.

👤Kwa mtazamo wa Kikristo, Mungu mwenyewe ndiye aliyewaandaa hivyo Waafrika kupokea wokovu kwa njia ya Yesu Kristo, aliyekuja si kutangua bali kukamilisha yale yote yaliyo mema katika binadamu wote.
 
Waafrika walimjua Mungu kabla ya ujio wadini alichofanya shetani ni kutake advantage ya waafrika kutojua Mungu yupi wanamuabudu akajivika u mungu kupitia mizimu.
Kabla ya ujio wa dini waafrika watakahukumiwa KWA sheria ya do and don't do natural justice sheria za asili.
 
Waafrika walimjua Mungu kabla ya ujio wadini alichofanya shetani ni kutake advantage ya waafrika kutojua Mungu yupi wanamuabudu akajivika u mungu kupitia mizimu.
Kabla ya ujio wa dini waafrika watakahukumiwa KWA sheria ya do and don't do natural justice sheria za asili.
Sio kwa wote. Soma hapa vizur utaelewa. Kwenye vitabu vya dini kuna majina ya wafu uwaga wanatajwa
 
Back
Top Bottom