Ukiishi bila unafiki kibongo bongo tarajia kupata anguko / hatuutaki ukweli

Ukiishi bila unafiki kibongo bongo tarajia kupata anguko / hatuutaki ukweli

BIOTOXINS

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2026
Posts
1,091
Reaction score
2,283
Mfumo wa maisha yetu kama watanzania unafikirisha sana ,sasa Huwa najiuliza .ni nani aliturithisha uongo, hapa nitatoa mifano kadhaa

1.mtu akikuomba chenji ukamwambia ninayo ila inanitosha Mimi ni kosa jibu lake > chenji sina ,na pole labda badae nitapata nikupe hili jibu mtu anaondoka akiwa na fraha

2.Ukimtongoza mwanamke ukamwambia ukweli mfano naumwa ugonjwa flani mfano ukimwi ni kosa> jibu lake anapaswa aelezwe uongo

3. Unamuazima mtu pesa labda nisaidie laki mbili nikanywee pombe mtu hakupi > badala yake unapaswa udanganye mfano unauguliwa ,au ndugu kapata ajali
Mifano ni mingi ninachojaribu kukutafta hapa kwa Nini tuukubali uongo na ukweli hatuutaki kisaikolojia ikoje ni mifumo ya elimu ,au inakuaje na nan alitutengeneza kuwa hivyo
Mwisho
Note mm ni form 4 point 29 2011 . Huwa napenda kutafakari sana kama nimekosea nisamehewe
 
Form 4 point 29 ni 4?

Ndio maisha yalivyo u can’t change it, kuna muda u have to fake it in order to make it! Ukijifanya muwazi sana utaishia kupoteza uaminifu na kusemwa vibaya na watu hata usiowafahamu!

Kama unahisi ni rahisi wewe kumpa pesa mtu akafanyie starehe, wakati wewe pia una mambo yako mwingine hawezi! Kwamba mwanamke akikwambia nina ukimwi utamkubali bila maswali basi uko vizuri! Kuwa loyal haina maana ya kuwa ufunguke kila kitu mengine baki nayo ila isiwe sababu ya kuwaumiza wengine!
 
Ni sawa ninachojaribu kuaza ,Nini kilitokea kisaikolojia imekaaje kwa nn tuukatae ukweli Yan mpaka tudanganywe why?
 
Kuna mwamba mmoja aliwahi kuniambia nimefanikiwa kujenga kakibanda kangu,aisee kwenda kuona kumbe ni bonge la Nyumba nikasema aloo! Unafiki bongo kwenye damu.
Duh nilitaka kulia, jamaa anasema twende ukaone nilipopanga matofali sio kujenga, sisi maskini hatujengi

Nilichoenda kukiona niliingia ubaridi, nilikutana na nyumba ya ndoto zangu
 
Kuna jamaa yangu aliniambiaga

"Daah tunapambana pambana kaka mambo bado"

Bqada ya muda nakuja kutambua kuwa ana supermarket,saloon ya kiume,saloom ya kike,restaurant,kiwanja zanzibar,amejenga kwao bonge la jumba,ana gari ....

Daah noma sana

#Ni tour guider anaongea lugha 4 ukipata time ya kusoma lugha piga kifaransa na italy au mwambie ndugu yako🙏
 
Kuna mmoja nilikuwa nasoma nae advance shule moja huko Mbeya campus shule x aisee jamaa muda wote analala darasani, akitoka kwenye mtihani anakwambia aisee hii paper mimi napata zero !

Matokeo yakirudi ana 97% au 98% alafu mwalimu anasema wewe tumetunga wote nini nikawa namuangalia tu kwa hasira jamaa anacheka tu.
 
Back
Top Bottom