Ukiishi bila unafiki kibongo bongo tarajia kupata anguko / hatuutaki ukweli

Ukiishi bila unafiki kibongo bongo tarajia kupata anguko / hatuutaki ukweli

Form 4 point 29 ni 4?

Ndio maisha yalivyo u can’t change it, kuna muda u have to fake it in order to make it! Ukijifanya muwazi sana utaishia kupoteza uaminifu na kusemwa vibaya na watu hata usiowafahamu!

Kama unahisi ni rahisi wewe kumpa pesa mtu akafanyie starehe, wakati wewe pia una mambo yako mwingine hawezi! Kwamba mwanamke akikwambia nina ukimwi utamkubali bila maswali basi uko vizuri! Kuwa loyal haina maana ya kuwa ufunguke kila kitu mengine baki nayo ila isiwe sababu ya kuwaumiza wengine!
Ibra wa kwenye biblia alidanganya wa misri kuwa Sara so mke wake bali dadake.... usisahau Ibra anaitwa baba wa imani..
 
Bongo nyoso
Ukimsikiliza bongo na kumwamini jiandae kuumia tu...

Na swala la mtu kukupa ahadi, Kamwe usitilie maanani bongo hubadilika kama kinyonga
 
Mfumo wa maisha yetu kama watanzania unafikirisha sana ,sasa Huwa najiuliza .ni nani aliturithisha uongo, hapa nitatoa mifano kadhaa

1.mtu akikuomba chenji ukamwambia ninayo ila inanitosha Mimi ni kosa jibu lake > chenji sina ,na pole labda badae nitapata nikupe hili jibu mtu anaondoka akiwa na fraha

2.Ukimtongoza mwanamke ukamwambia ukweli mfano naumwa ugonjwa flani mfano ukimwi ni kosa> jibu lake anapaswa aelezwe uongo

3. Unamuazima mtu pesa labda nisaidie laki mbili nikanywee pombe mtu hakupi > badala yake unapaswa udanganye mfano unauguliwa ,au ndugu kapata ajali
Mifano ni mingi ninachojaribu kukutafta hapa kwa Nini tuukubali uongo na ukweli hatuutaki kisaikolojia ikoje ni mifumo ya elimu ,au inakuaje na nan alitutengeneza kuwa hivyo
Mwisho
Note mm ni form 4 point 29 2011 . Huwa napenda kutafakari sana kama nimekosea nisamehewe

Mfano mwingine,

Mtu unayemweshimu anakukopa, unaweza tu kumwambia sina hiyo bajeti, unaanza maelezo ela zipo Bank, ATM kaondoka nayo wife, sasaaa, embu nicheki mida ya saa kumi hivi. Saa kumi inafika na simu unazima. Ungesema sina hiyo bajeti usingezima simu.
 
Lakini si tulikubaliana waongo na wanafiki hawataurithi ufalme wa mbinguni? Mkasema yeye aliyesema usiue ndiye huyo huyo aliyesema usiseme uongo.

Ila sasa napata wakati mgumu kwasababu hata Yakobo alidanganya ila akaja kubarikiwa baadae..🤔
 
Back
Top Bottom