Ukiishi kwa ndugu, rafiki, jirani zingatia haya

1. Usisahau kusaidia vi Junior na Precious homeworks
2. Kupaka kiwi viatu vya baba mwenye nyumba if necessary.
3. Usikorome usiku
4. Jifanye huna shobo na msosi, hasa nyama chukua tu pande tu dogo wao ndio waseme ongeza.
5. Saidia kazi ndogo ndogo za nyumbani
 
Uliwaona hawana akili sio, ukishakuwa mtu mzima ndio unaona jinsi maisha yalivyo na changamoto nyingi.

Mtu yupo na watoto wawili, lakini amepanga room moja achilia mbali mwenye uwezo wa kupanga nyumba nzima. Haya maisha oneni tu yalivyo.
Wewe acha tu ,hata baba yangu mzazi nilikuwa nikimlaumu sana katika mambo mengi,Father kakosea hapa , Father kafanya kile alitakiwa afanye hivi,sasa leo hii yale ambayo baba yangu alifanya akiwa na miaka 33 mimi nina 40 sijayafikia.
 
Mfano kazi gani zitakufanya ushushe heshima?
 
Wakiwa wagonjwa tena? Waje kumsumbua malkia wake aanze kuwauguza? Hapo ndio hawatakiwi kabisa
 
Fanya hima usikae muda mrefu kwa ndgu yako mkuu.

Pamoja na yote uliyoshauriwa jitahidi hilo mkuu, ukishindwa bora urudi bush tu.

Kwa ndgu maneno unayosemwa ni mengi japo huenda usiyasikie lakini sio ndgu wote watapenda wewe kukaa pale.
 
Huyu nae alikuwa mwehu, wenzie kipindi cha uchumba wanafichaga makucha
 
Watu mjini, umasikini unatusumbua. Huko kwa rafiki zangu wasukuma, ukienda ukawa mgeni wao alafu ukala kidogo inakua ugomvi.

Watu wamejaza ndani gunia za mchele, mahindi, na mifugo ya kutosha. Huko kwa wakurya, hata kwa jirani wewe unapiga msosi vizuri tu na wala hakuna anaeshangaa. Shida inakuja kwa watu wa mjini haswa Dar.

Pambaneni wakuu, wageni wakija waishi vizuri. Weka chakula cha kutosha ndani ili kusiwepo na habari ya kumhesabia mgeni idadi ya vijiko anavyopakua.

Hayo mengine sipingi wala siungi mkono!
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bro kaza sana isiwe na matarajio makubwa kwa ndugu yeyote Yule mi binafsi sijawai kusafiri na kukaa kwa mjomba ,kaja, dada, mama mdogo sijui mkubwa zaidi ya kwenda kwa bibi tu yaani nafikia kwa bibi basi sijawai kukaa kwa mtu

Nilipoanza chuo nilifikia kwa uncle nikaa miezi 2 kwa shida sana analazimisha nibaki ila nikaondoka ila sikuwa nataka kufikia kwa mtu na walikuwa wananipigia simu mpaka kunifuata nilipopanga ila leo ndo nimekuwa Kama mtoto wao nawasaidia sana walicheza na bahati sana wakiwa na shida tu wananiona mpaka kodi nawaboost hata miezi miwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…