Ukiitwa na Rais Ikulu Kwa mazungumzo rasmi ukakataa utafanywa nini?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Endapo Rais WA nchi akakuita Ikulu Kwa mazungumzo ukakataa kwenda kumsikiliza Kuna madhara yoyote unayoweza kuyapata?

Ukitii unaweza ukamsikiliza na baada ya kumsikiliza ukaona anataka kukutoa Kwenye msimamo wako unaweza kumkatalia?

Ukimkatalia ukabaki na msimamo wako vyombo vya usalama vya kiafrika vitakuacha salama?

Kama havitakuacha salama, uhiari wa mwananchi kuitwa kuonana na Rais upo wapi au ndo Ile kusema Mhe. Rais huku Afrika ndiye MWENYE maamuzi ya wewe umpende hata kama moyoni unamchukia?

Lini tutapata Rais ambaye atatumbua kumwita mwananchi akakataa siyo Kosa la jinai? Lini tutapata Rais asiyeamini kumfunga yeyote MWENYE mawazo kinzani?
 
Mbowe yupo huru hayo menginee achana nayo ,nchi n yetu sote tuijenge kwa pmj kuitwa na raic n jamboo la heri maana wameenda kuongea nakujadili mambo yakuhusu nchi jinc yakuitoa hapa ilipoo nakwendaaa mbelee ,mbowe asamehe na maisha yaendeleee tunamtegemea atupambaniaa tupate KATIBA MPYA
 
Si vizuri kukataa na siyo ustaarabu unless kuwe na sababu kubwa sana...

Mfano Nabii Eliya aliwahi kuukataa wito wa mfalme Ahazia kwenda Ikulu kuonana naye kwa sababu nia na kusudi la Mfalme Ahazia dhidi ya Nabii Eliya halikuwa jema...

Sababu ya Nabii Eliya kutakiwa kufika Ikulu ya Mfalme Ahazia ilikuwa ni baada ya kuhoji na kukosoa maamuzi ya Mfalme kuomba au kuabudu shetani Baalzebuli badala ya Mungu wa Israel aliye hai - Yehova kiasi cha huyo mfalme kuona amedharauliwa...

Habari hii utaipata kwenye biblia kitabu cha 1 Wafalme 1: 1 - 15

Kwa hiyo, jibu inategemea.

Kwamba ukikataa utafanywaje?

Ofcoz, kwa mfalme (Rais) dictator tegemea adhabu kali ya waziwazi au ya kimkakati bila wewe kujua kuwa kuna mkono wa shetani unakupiga mdogo mdogo...!
 
Mzazi/Mlezi wako akikuita utakataa? Labda anataka akakukabidhi wosia naye ck sake zimeenda
 
Lile Paka jike linauzi.Hakuna jinsi wataweza kunyong'oneza upinzani Tanzania.

Huwezi kumtesa mtu kwa miezi saba bila sababu yoyote ile kisha leo ujifanye kukutana nae kinafiki kwa kisingizio cha kujadili siasa za kistaarabu.She is hopeless sinner.Kudai katiba mpya ni siasa zisizo za kistaarabu?
 
Kalale wewe kesho Sabato
 
Endapo Rais WA nchi akakuita Ikulu Kwa mazungumzo ukakataa kwenda kumsikiliza Kuna madhara yoyote unayoweza kuyapata?

Ukitii unaweza ukamsikiliza na baada ya kumsikiliza ukaona anataka kukutoa Kwenye msimamo wako unaweza kumkatalia...
Subiri siku ukiitwa....ukatae tutajua hapo....nini kitatokea
 
Future Impossible Tense
Huwezi kuitwahamna haja ya kujadili
 
Rais ikiwa atakuita yeye kama yeye unataamua ww kwenda au kutokwenda. Ila ikiwa mamlaka yake ikikuita hapo lazima uende na usipoenda ni kosa kisheria.

Mfano ni hakimu akikuita binafsi nyumbani kwake sio lazima uende ila akiwa na koti la mahakama akikuita(wito wa mahakama) lazima uende na usipoenda tabu iko palepale.

Kwa mfano juzi aliniomba jirani yangu kumsaidia kuingiza ndani mifuko yake ya mbolea ila mm sikuenda na hajanifanya chochote labda mbele huko NIKIJICHANGANYA na kama atatunza kisasi chake atanikomoa ila kwa sasa I am FREEEEEEE.
 
Endapo Rais WA nchi akakuita Ikulu Kwa mazungumzo ukakataa kwenda kumsikiliza Kuna madhara yoyote unayoweza kuyapata?

Ukitii unaweza ukamsikiliza na baada ya kumsikiliza ukaona anataka kukutoa Kwenye msimamo wako unaweza kumkatalia?

Ukimkatalia ukabaki na msimamo wako vyombo vya usalama vya kiafrika vitakuacha salama?

Kama havitakuacha salama, uhiari wa mwananchi kuitwa kuonana na Rais upo wapi au ndo Ile kusema Mhe. Rais huku Afrika ndiye MWENYE maamuzi ya wewe umpende hata kama moyoni unamchukia?

Lini tutapata Rais ambaye atatumbua kumwita mwananchi akakataa siyo Kosa la jinai? Lini tutapata Rais asiyeamini kumfunga yeyote MWENYE mawazo kinzani?
Kwanza mpaka upate mwaliko wa Rais Ikulu ujue kua kulikuwa na mazungumzo mengine yaliyokuwa yanaendelea chini kwa chini .Uwezi kuonana na Rais ghafla tu bila kuwa na taarifa na hilo. Kwa hiyo swala la kukubali au kukataa kuonana naye ni jambo ambalo mtakubaliana kabla ya kupata mwaliko.
 
Endapo Rais WA nchi akakuita Ikulu Kwa mazungumzo ukakataa kwenda kumsikiliza Kuna madhara yoyote unayoweza kuyapata?

Ukitii unaweza ukamsikiliza na baada ya kumsikiliza ukaona anataka kukutoa Kwenye msimamo wako unaweza kumkatalia?

Ukimkatalia ukabaki na msimamo wako vyombo vya usalama vya kiafrika vitakuacha salama?

Kama havitakuacha salama, uhiari wa mwananchi kuitwa kuonana na Rais upo wapi au ndo Ile kusema Mhe. Rais huku Afrika ndiye MWENYE maamuzi ya wewe umpende hata kama moyoni unamchukia?

Lini tutapata Rais ambaye atatumbua kumwita mwananchi akakataa siyo Kosa la jinai? Lini tutapata Rais asiyeamini kumfunga yeyote MWENYE mawazo kinzani?
walishaomba kukutana nae mapema sana alipoingia tu ikulu,kama kamwita wakajadili kuna ubaya gani? Alianza na makamu wake na sasa mwenyekiti mbowe,mataifa ya nje walitaka hii kesi ifutwe viongozi wadini nawakataka upatano nandohilo limefanyika hii ni nchi yetu sote
 
Endapo Rais WA nchi akakuita Ikulu Kwa mazungumzo ukakataa kwenda kumsikiliza Kuna madhara yoyote unayoweza kuyapata?

Ukitii unaweza ukamsikiliza na baada ya kumsikiliza ukaona anataka kukutoa Kwenye msimamo wako unaweza kumkatalia?

Ukimkatalia ukabaki na msimamo wako vyombo vya usalama vya kiafrika vitakuacha salama?

Kama havitakuacha salama, uhiari wa mwananchi kuitwa kuonana na Rais upo wapi au ndo Ile kusema Mhe. Rais huku Afrika ndiye MWENYE maamuzi ya wewe umpende hata kama moyoni unamchukia?

Lini tutapata Rais ambaye atatumbua kumwita mwananchi akakataa siyo Kosa la jinai? Lini tutapata Rais asiyeamini kumfunga yeyote MWENYE mawazo kinzani?
Kuitwa na Rais ni sheria.

Ukikataa unashtakiwa.

Ndio maana naniliu wa Mtama alienda Ikulu huku analia!
 
Raisi ni mkuu wa nchi na kiongozi mkuu wa serikali hivyo wito wake ni bahati sio kila mtu anapata hiyo chance,mi nikiitwa na bosi wangu naenda mbio mbio[emoji23][emoji23] nikiitwa na Raisi sijui itakuwaje.
 
Rais anatoa,"Mwachie huru Mbowe sasa hivi."
Halafu Mbowe aitwe Ikulu akatae?
 
Unachokisikia public ni vile ambavyo tayari vimeshakubaliwa na pande zote mbili...

Ville visivyoenda sawa hutakaa uvijue...
 
Kwa Tanzania ( ya sasa) unaweza shtukia umevamiwa, kubebwa na kulazimishwa kwenda na kukupiga picha kama Ndugai …
 
Back
Top Bottom