Tusijifungie sana ndani. Tuwe na kawaida ya kudunduliza pesa kwa ajili ya kusafiri nchi za mbali huko na kutazama maisha kwa upande mwingine.
Kusema ukweli, ukiwa sio mtu wa kupangilia mambo yako hutafurahia maisha wala hutaifaidi dunia ipasavyo. Pesa tu ndio ikufanye usiende mataifa mengine kupumzika na kubarizi? Jitafakari upya.
Kwa mfano, mwezi wa 5, 6 na 7 ni kipindi kizuri kwenda nchi za Ulaya hususani Ufaransa na Roma.
Sio hizo tu; kuna Ubelgiji, Uholanzi, Uswizi, Ujerumani, Austria Italy hasa kule Vatican City n.k.
Ukijichanga ukapata kama Milioni 6 tu hivi utaweza kufanya ziara katika nchi zote hizo, utaenjoy, utalala, utakula, utatembelea vivutio, utapiga picha nzuri za kumbukumbu na utarudi Tanzania kwa bajeti hiyo tu tena utakaa kwa muda wa wiki 2 mfululizo.
Hapo ugumu uko wapi?