Ukijipanga vizuri, mwaka huu unaweza kwenda Ulaya kufurahia maisha

Tusijifungie sana ndani. Tuwe na kawaida ya kudunduliza pesa kwa ajili ya kusafiri nchi za mbali huko na kutazama maisha kwa upande mwingine.

Kusema ukweli, ukiwa sio mtu wa kupangilia mambo yako hutafurahia maisha wala hutaifaidi dunia ipasavyo. Pesa tu ndio ikufanye usiende mataifa mengine kupumzika na kubarizi? Jitafakari upya.

Kwa mfano, mwezi wa 5, 6 na 7 ni kipindi kizuri kwenda nchi za Ulaya hususani Ufaransa na Roma.

Sio hizo tu; kuna Ubelgiji, Uholanzi, Uswizi, Ujerumani, Austria Italy hasa kule Vatican City n.k.

Ukijichanga ukapata kama Milioni 6 tu hivi utaweza kufanya ziara katika nchi zote hizo, utaenjoy, utalala, utakula, utatembelea vivutio, utapiga picha nzuri za kumbukumbu na utarudi Tanzania kwa bajeti hiyo tu tena utakaa kwa muda wa wiki 2 mfululizo.

Hapo ugumu uko wapi?
Naomba mchanganuo fasta

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Hivi vitu muwe mnaongea kwenye semina za wakurugenzi, hapa wengine mnatuonea jamani
Wala usitishike mimi nipo huku usukuman kuna wazee wana mihela yaani something like 30 t0 50 milion zipo ndani na wala hutosikia kasafiri labda Akiumwa ndo utasikia kaenda mwanza ujue huko ni bugando au ukisikia yupo DSM ujue yupo mhimbili au mloga nzila vinginevyo utasikia yupo Katavi au Kigoma kuangalia ng'ombe zake.
Waweza pia sikia yupo Morogoro kumbe kaenda angalia mashamba yake ya mpunga. Kiukweli pamoja na hela zake nyiingi but still too primitive and crude kwa hiyo shida siyo hela wengine ni kujitambua tu.
 
Sahihi kabisa
 
Wewe unamuona primitive ila yeye ana furaha na amani tele, cause hayo mazingira yake ndio yamefanya apate huo ukwasi
 
Back
Top Bottom