Ukikuta begi limetelekezwa limejaa maburungutu ya pesa liache kama lilivyo, usijizidi akili kujiona mjanja ukimbie nalo

Ukikuta begi limetelekezwa limejaa maburungutu ya pesa liache kama lilivyo, usijizidi akili kujiona mjanja ukimbie nalo

Uzuri wanaotafuta hilo begi hawatumii helcopta na cha kuokota si cha kuiba.....nazichukua vizuri tu na begi naliacha nakuwa nabadilika badilika kama saa yaani kwenda hapa nakaa dakika 5 napekenyua kitita kimoja baada ya kingine naweka kando, naondoka tena nakwenda kwingine tena nakaa dakika 5 napekenyua fedha zilizobaki alafu na change tena location (hicho kidude (gps) kama kipo kwenye bundle la hela nakiacha hapo hapo na burungutu moja ya kujazia mafuta.

By the way hizi ni simulizi na hakuna mtu ataweka gps kwenye burungutu la fedha ili iweje yaani maana ukitoa fedha ni kwenda kuzitumia hizo purukushani za gps za nini, labda kama zinasafirishwa kutoka bank kuu kwenda mkoa mwingine
 
Sema mwamba katoa kama tahadhari ila kuna baadhi wamemchukulia poa.. ila omba isikukumbe hii, ni kweli kuna vi trackers ni vidogo sana kuvinotice ni mtiti kuna vingine vimekaa kama stickers so kama mwenye pesa aliweka hako na akaamua kukutrack na hujui atakudaka..
 
Tume shtuka we ni njagu ume tumwa uhamasishe ujinga humu
 
Chukua peleka bank unless una wasi wasi sababu fedha ni nyingi na huna huo mzunguko bank ndo tumia akili nyingine ikiwemo ya kuzigawa mara tatu mpaka sita na kuzificha sehemu tofauti tofauti.
 
Movie sio uhalisia japo tracker zipo wahuni wanakamatwa sana majuu
 
Begi ukilikuta njiani kuna uwezekano mkubwa wa uhalifu kuhusika, aidha limetupwa wakati majambazi yakimkimbiza mwenye nalo, majambazi waliiba ila wakalitupa kupoteza ushahidi hasa wakiwa suspects, wezi wameiba pesa na ghafla wanaona kuna ukaguzi barabarani, n.k.

Maisha ya hapo zamani mtu akikuta begi kama hili na kuliacha, watu walimshangaa sana kwamba kapitwa na bahati na bahati haiji mara mbili,

Ila kwa siku hizi mtu akiliacha begi kama hilo ana akili sana, wala si wa kumcheka.


Teknolojia ya GPS tracking imekuwa kubwa sana, Begi lenye maburungutu ya hela ni kawaida sana kuwekwa gps inayoonyesha movement zote za begi, Gps ndigo ya ziada inaweza kuwekwa kwa ustadi katikati ya pesa zilizobanana, hata begi likitupwa location ya mzigo inaonekana.

Gps trackers itaonyesha sehemu lilipo begi na movements zake, hivyo ukiliokota na kwenda nalo nyumbani kwako, watajua lilipo na kulifuata, kibongo bongo utapewa kipigo kikali sambamba na kupewa kesi ya ujambazi.

Watu wanaweka gps kwenye pikipiki na magari na yakiibiwa wanayapata sembuse mabegi yenye maburungutu ya hela ? hilo swali ujuilize sana.

Njia pekee ya kuiba hilo begi labda uwe na jammer wanazotumia majambazi wa kisasa kuiba pikipiki na magari, gps jammer ni kifaa maalum cha kublock mawimbi ya gps tracker.

Begi ukikimbia nalo kwa muda mfupi ukiwa na furaha utasema maisha umeyapata lakini kifuatacho baada ya hapo kinaweza kufanya maisha yako yawe ya majonzi sana.
Usitutishe
 
Chukua pesa wahi chap kwa wakala nmb crdb fanya muamala potea
Usituletee ugogolosh
 
Back
Top Bottom