Ukikutana na Rais Samia kero gani kubwa utamwambia unayoiona mtaani kwako?

Ukikutana na Rais Samia kero gani kubwa utamwambia unayoiona mtaani kwako?

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Wakuu,

Imagine, upo katika moja ya mkutano wa Mhe. Rais na ukapata nafasi ya kuuwakilisha mtaa wako kufikisha kero kwa mheshimiwa Rais wa nchi hii.

Unafikili wewe kama mwakilishi wa wanachi wa mtaa wako utataja kero gani?

Kutuwakilisha kwako ndio ufumbuzi wa kero na matatizo yetu mtaani

Tiririka.
 
Mwanshambwa luka kesha tusema kero zetu zote kwa mamake nkikutana na mama ntamwomba hela ya koncho tuu
 
Kero yangu ni vumbi na joto

Kwakweli serikali iangalie haya mambo kwa jicho la tatu sababu hapa mtaani kwetu joto na vumbi vimekua kero sana alafu serikali tukufu ya mama Samia ipo kimya tu
 
Kero yangu ni vumbi na joto

Kwakweli serikali iangalie haya mambo kwa jicho la tatu sababu hapa mtaani kwetu joto na vumbi vimekua kero sana alafu serikali tukufu ya mama Samia ipo kimya tu
😂😂 Mkuu hyo ya vumbi angalau atatuma gar limwage maji au kuweka lami kasheshe kwenye joto ndo changamoto ila unaweza shangaa akakwambia ataitatua pia ya joto
 
Aache kulea nchi km Mama wa nyumbani. Kuna kauli zake mfno

'Nendeni mkalitizame' inaniudhi

Utafkiri hana maamuzi
 
Vijana hatuna hela ya kutoa mahari tuowe tunaishia kusema ndoa mbaya kwa saba u hatuna hela.
Hivyo basi mimi kama senior bachelor tungeomba serikali sikivu ya mama watupe hela za mahari tuoe tumechoka na nyeto za mlenda vuguvugu
 
Mi sitamuambia kero za mtaani kwangu mi nitamuambia kero ambayo itaamua matatizo mengi ya nchi hii!, kwanza abane matumizi ya fedha serikalini pili aanzishe vyanzo vitakavyoingiza pesa nyingi serikalini tatu pesa iliyoingia ahakikishe inafanya kazi inavyotakiwa nakutuletea tija kwenye nchi!.

Tena nimuelekeze kabisa pesa atatoa sehemu hizi..
Madini
Biashara hapa akiboresha mazingira ya biashara kuna pesa nyingi mno!.
Kilimo na ufugaji, wasiseme serikali haifanyi biashara!, serikali inaweza Tanzania ina 70% ya ardhi inafaa kwa rutuba kama wao hawawezi wawape wawekezaji wa ndani, pia nchi imezungukwa namaji yakutosha kulia njaa ama ukame ni aibu!.

Utalii hapa siongezi chochote ye mwenyewe anaelewa uzuri katokea Zanzibar!.

Tatu anatakiwa auze watu wake maswala ya ajira yatakoma!, kuuza watu kwa maana hii vijane wafundishwe skills sio tena elimu ya kidubwasha hii imekaa kimchongo sana!, fani ya IT inahitaji watu wengi sana na hawa wakiwa na utaalamu wakutosha wataisaidia nchi hata siku ikukumbwa na attack ya cyber kubwa!, kusema kweli mi nina wasiwasi ipo siku hii nchi tutakuja kulia na technology sikumoja tutalizwa wengi mno, naona kuna holes nyingi watu mpaka leo bado wanalizwa na pyramid scheme hahaha!!..😅

Nimechoka kuandika ila akazie hivyo atanishukuru!
 
Vijana hatuna hela ya kutoa mahari tuowe tunaishia kusema ndoa mbaya kwa saba u hatuna hela.
Hivyo basi mimi kama senior bachelor tungeomba serikali sikivu ya mama watupe hela za mahari tuoe tumechoka na nyeto za mlenda vuguvugu
kero hii naijibu mimi hapa hapa,vijana msiendekeze mapenzi,badala yake mjikite sana katika kilimo,tuna ardhi yenye rutuba karibu mikoa yote katika nchi hii, na serikali kila msimu inatoa mbegu na mbolea za ruzuku kwa wananchi,wewe mzabzab na vijana wengine kama wewe ukilima ekari mbili kwa miaka mitatu, utakakuwa tayari umepata hela ya kuolea. Tusilaum kila kitu serikali.
 
Mabango ya picha zake yamechafua sana mitaa
hapa tuwe tunajibu kama watu wenye akili na tunatazamana na mh. Mwenyewe,manake unapewa mic mkutanoni unasema jambo kama hili ulilolisema wewe kweli? Hapa utaishia mikononi mwa vyombo vya dola haraka sana.
 
Back
Top Bottom