Ukimiliki laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja utalipa faini Tsh 5M au kufungwa gerezani kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja kuanzia 1 Julai, 2020

Ukimiliki laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja utalipa faini Tsh 5M au kufungwa gerezani kwa miezi 12 au vyote kwa pamoja kuanzia 1 Julai, 2020

Logically hii kitu haipo sawa. Kama nimesajiri line tatu shida yao nini? Nani kaenda kulalamika?

Anyway, kama wana shida nazo saaana wao wadeal na kampuni za simu na sio watumiaji maana hao ndio waliosajiri huku wakiona kwenye system kwamba tayari mtu huyo ana line nyingine ya mtandao husika
 
Nadhani hapa TCRA wamekosea au Teknolojia imewaacha nyuma. Yaani kama mwananchi anaona vodaxom ndio mtandao mzuri na ana simu 2 hii nayo ni ya kutungia sheria kweli kumtoa kwenye umiliki wa line?

Nadhani system automatically ingedelete hizo namba kuliko kusumbuana dunia inakwenda mbele sisi tusirudi nyuma.

Let say mtu ana simu ndogo ya tochi na ana smart zote voda huyu ameshakiuka sheria. Hizi sheria zilipitishwa na wabunge gani wenye elimu gani na uelewa gani no wonder bado tuko nyuma kimaendeleo sababu ya upeo wa kufikiri mdogo. Tunaelekea china sasa na huu ukomunisti wao wenyewe hawajauweza bado mpaka wanakuja huku kuuza yeboyebo huwezi kuona mwingereza kaja kuuza yeboyebo sababu ya capitalism kwao.
 
Tatizo tu mitanzania ni mitahaira Fulani hivi.kwanini tusiamue wote kuwa na laini moja ya mtandao mmoja tu tutakaouchagua ili mitandao mingine ife ili hao tcra wapate furaha zaidi.
Huna akili
 
Wewe ndo hujaelewa! Hiyo text aliipokea imetoka kwa mtoa huduma wa mtandao anaoutumia ambapo kwa mujibu wa kumbkumbu za mtoa huduma zimesajiliwa SIM CARD zaidi ya moja kwa namba yake ya NIDA kwa mtoa huduma huyo huyo.
 
Bwashee kabila langu linaingiaje hapo!
Ulisema line zako zilikuwa na ‘mikopo’ na ukaenda ofisini ili kuzifufua, ulichokwama ni majina matano tu ila lengo lako ilikuwa kuzifufua!
Ok Sorry basi Mkuu SIAJKUTAJA KABILA (ww umetumia Bwashee)
lkn post yangu hukuielewa maana nilimQuote kwa kumjibu mleta Mada kuwa nilifanya MAKUSUDI kutaja namba za uongo ili NIFUNGIWE na nikatoka kichwa chini kwa furaha
bora wewe hukuathirika kwa faida mm nilikuwa na line 2 na zina mikopo mikubwa tu zikapotea nikawafuata ili nifufue, wakaniuliza majina ma5 du nikakosea wamenitisha kuwa hawawezi kuzifufua kabisa nilitoka nimeinama na SIZIFUFUI.
 
Nina swali hata laini za uwakala nazo zinatakiwa kutolewa maelezo au inakuwaje hapo
 
Sheria ngumu sana. Nawaza kosa linakuwa wapi,simu nainunua mimi,line yangu.

Hii inchi ina viongozi wapuuzi sana,kisa tu watu kuwasajilia wenzao namba za simu. Hawajui tatizo ni kutokutoa NIDA ID kwa raia wote.

Mimi Nina laini zifuatazo,
Voda 4 hapa ninatumia 3 moja anatumia mama angu
2 tigo zipo 5 zote natumia mimi mwebyewe
3. Airtrl moja ambayo natunia pia
4. Halotel 1 kwa sasa siitumii
N.b laini anayotumia mama ni yangu Na sidhani kama ni haki kunizuia kuwasiliana Na mzazi kisa namba ya simu yangu kuiweka kwenye simu yake nchi hii INA mengi ya kufanya Na so huu upuuzi wanaotuletea.
 
Ndio kupunguza gharama za kupiga. Waweza kuwa nazo laini hata nne za mtandao mmoja kupunguza gharama za kuwasiliana ya kwanza ya ofisi ya pili ya nyumbani ya tatu yako mwenyewe ya nne ya mwanao ambaye hajafikia umri wa kuwa na kitambulisho cha taifa ili asajiliwe anayesoma tuition mbali.

kwa mwendo huu naona kama itakuja sheria ya kupiga marufuku mtoto chini ya miaka 18 kushika simu
 
Huu ni ujinga na UONEVU tusipangiane jinsi ya KUISHI..
SIMU YANGU NANUNUA LAINI KWA PESA ZANGU.
Cha muhimu ni kuwa ni sahihi kwa JINA LANGU

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Kwani kuna ulazima gani wa kumiliki laini nyingi za mtandao mmoja?
Hapo nawapongeza TCRA.
Kama ni kweli hujui ulazima iko hivi,

Mimi nina SIM moja ya vodacom ninayoitumia mwenyewe, nina SIM nyingine ya vodacom kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, hii inakua nyumbani ili niweze kuwasiliana na watoto ninapokua kazini

SIM nyingine ya tatu naitumia kwenye chumba cha utotoleshaji wa vifaranga (Hatch room) ili kupata taarifa umeme unapokatika

Wapo watu wana shughuli nyingi zaidi na hivyo inawalazimu kuwa na hata SIM 10
 
Kama ni kweli hujui ulazima iko hivi,

Mimi nina SIM moja ya vodacom ninayoitumia mwenyewe, nina SIM nyingine ya vodacom kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, hii inakua nyumbani ili niweze kuwasiliana na watoto ninapokua kazini

SIM nyingine ya tatu naitumia kwenye chumba cha utotoleshaji wa vifaranga (Hatch room) ili kupata taarifa umeme unapokatika

Wapo watu wana shughuli nyingi zaidi na hivyo inawalazimu kuwa na hata SIM 10

Muhimu mimi ninafikiri ziwe zimesajiliwa kwa alama za vidole na ziwe zinalipiwa malipo yote yanayostahili . Sidhani kama yupo mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya uhalifu kwa kutumia line alizosajili kwa jina lake na taarifa zake zote ambazo ni ushahidi tosha dhidi yake pindi atakapokamatwa
 
Back
Top Bottom