Ukimkimbiza kichaa wote mtakamatwa kama vichaa ili msilete fujo kwa sababu watashindwa kuwatofautisha

Ukimkimbiza kichaa wote mtakamatwa kama vichaa ili msilete fujo kwa sababu watashindwa kuwatofautisha

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
471
Reaction score
1,217
Hii Dunia tupo watu wenye haiba mbali mbali rahisi na ngumu katika kuishi na wengine na bahati mbaya kuna haiba hazibadiliki wala kurekekebishika hivyo unachotakiwa ikiwa utakutana na mtu mwenye haiba hiyo ni kujifunza kuishi naye au kumpuuza tu

WAKIKUTA UNABISHANA NA KICHAA WATAKUSHANGAA WEWE KWA SABABU TAYARI WANAMJUA YEYE NI KICHAA 😔

Fuatilia hao wanaokunyima usingizi mpaka kuhatarisha afya yako kwa kupata magonjwa ya moyo na shinikizo la juu la damu utakuta wengi wao walishashindikana huko watokapo hivyo upo unapambana na watu ambao ndivyo walivyo.

MTU KASHINDWA KUBADILISHWA NA WAZAZI/NDUGU ZAKE KWA MIAKA 30 UNADHANI UTAMUWEZA NDANI YA MWAKA MMOJA?

UNAPOTEZA NGUVU KUTAFUTA SULUHU KATIKA WATU AMBAO WANAFURAHIA VURUGU.

KATIKA ZAMA HIZI KUNA WATU NI LAZIMA UWAPUUZE TU LA SIVYO KILA SIKU UTAKUWA MTU WA MSONGO😔

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako
 
Kwaiyo CCM kichaa watanzania Tuachane nayo au tusibishane nayo Au.
 
Mbaya zaidi yule kichaa ndio huonekana Ana akili timamu ila ww mwenye akili timamu ndo utaonekana kichaa
 
Kichaa ni kichaa tupunguze taharuki
 
Back
Top Bottom