Ukimkiri Mungu na kumtumaini kamwe hawezi kukuangusha

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477


Your browser is not able to display this video.

Ruto alimkiri na kumtumaini Mungu hadharani, matokeo yake mwulize Uhuru Kenyata na Raila Odinga.

Magufuli alimkiri pia Mungu mbele ya dunia yote kuwa Mungu atatuponya na corona wala hakuna haja ya chanjo na barakoa! Leo hii Watanzania tuko salama wakati dunia imepita kwenye hali ngumu sana!! Watanzania tumwamini na kumkiri Mungu naye atanyosha mapito yetu!
 
Kumtamka Mungu mbele ya hadhara sio kumkiri Mungu. Acheni upotoshaji wa kijinga.
 
Alikokwenda Magufuli ni mbinguni ambako ni kuzuri sana kuliko duniani hata ukimpa fyrsa ya kurudi duniani hatakubali.
Hili linapunguza uwajibikaji kwa kuwaza kuna sehemu nzuri zaidi ya hii unanyoiona, watu wanajiandaa kunyakuliwa badala kupambana tufurahi maisha hapa duniani
 
Tusihame kwenye muktadha wa mjadala, muktadha ni kuwa Mungu ananguvu ya kumpigania mtu dhidi ya wapinzani wake au maadui wake hata kama hao wapinzani au maadui kibinadamu wanaonekana kuwa na nguvu sana!

Tukumbuke jinsi Daudi alivyomwua Goliathi kwa kuwa alimtumaini Mungu. Alimkabili Goliathi kwa Jina la Mungu wa majeshi!

Huu mfano wa Ruto dhidi ya Uhuru Kenyata ni mfano wa wazi ulio karibu na wa dhahiri sana!!
 
Mwanasiasa kama mtu anaweza kumwamini Mungu pia, hilo limedhihirishwa hadharani na Magufuli na Ruto! Imani inahusiana na watu wote wakiwemo wana siasa!!
Wanamtaja Mungu kwa maslahi binafsi na si kwa uchaji na uvuvio wa kweli wa kiroho.. In fact wengi wao mikono yao inanuka damu isiyo na hatia na wamejawa na udhalimu mwingi
 
Acheni Ujinga Ujinga Huo. Mnafanya Akili zenu zionekane ni Mgando.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…