Kama utafuatilia kwa makini maelezo ya lt Urio utagundua kesi hii ya Mbowe na makomandoo wa JWTZ ( wastaafu) ilipaswa kuwa ya Uhaini siyo Ugaidi.
Kutwaa madaraka kinyume cha katiba ya JMT kwa kutumia wanajeshi ni uhaini.
Urio anakiri Mbowe aliomba msaada wake ili CHADEMA itwae madaraka wananchi wasiendelee kuishi kwa mateso na unyonge.
Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Mwambie bosi wako kuwa hii movie alitakiwa kuajiri Director kutoka CIA au MIG16 au MOSSAD. Watu waliotumika hawana uwezo wa kutengeneza script zilizo karibu na ukweli. Actor aliyeandaliwa hana uwezo wa kukariri script wala kupresent sura ya huruma.
1. Hakuna mfano wa nchi duniani iliyopinduliwa kwa kukata miti na kuchoma vituo vya mafuta.
2. Tanzania kabla ya 2020 imewahi kushuhudia haya yafuatayo
A. Miaka 5 bila ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi.
B. Mauaji holela, maiti zilikuwa zinaokotwa coco beach, watu walikuwa wanatekwa na wengine kupotea, watu wamepigwa risasi
C.Watu walibomolewa nyumba zao bila fidia
D. Watu walifukuzwa kazini bila utaratibu wala kufuata sheria
E.Watu walinyanganywa fedha zao hata ambazo zilikuwa benki na biashara zao zikafanyiwa robbing hasa wale wa bureau de change
F.TRA walibambikia watu kodi zisizo lipika
G.Chaguzi ziliibiwa
H.Watu walishushwa mishahara kiholela
I. Masoko yalichomwa moto na biashara kuvunjwa
J.Milipuko ya mabomu
Kama vyote hivyo hapo juu havikuwahi kusababisha hata maandamano ni muujiza gani ungetokea ili kuchoma vituo vya mafuta na kukata miti kusababishe nchi kutokutawalika?
3. Tanzania kwa ukubwa wake ili kuuleta taharuki inakuhitaji kufanya jambo litakalo chukua karibu mikoa 16-20 kwa wakati mmoja? Je watu wanne wangeweza vipi kuratibu matukio katika ukubwa huo.
4. Kama kweli Mbowe alitaka kupindua nchi basi watu sahii wa kuwatumia walikuwa wanajeshi waliopo kazini sio wastaafu au waliofukuzwa.
5. Kama Mbowe angelitaka kuchukua nchi asingelimshikisha mtu kama Urio wakati ana ndugu jeshini
6. Kama Mbowe angelitaka kupindua nchi kama unavyosema basi mtu sahii wa kumzuru alikuwa Magu na sio Sabaya sababu Sabaya ni sisiminzi mbugani hana effect yeyote kwenye uongozi au Selikari ya nchi hii. Hivyo kumzuru Sabaya kusengeleta taaruki yeyote ile sio tu nchi bali hata Hai kwenyewe.
Kihistoria mapinduzi yote Afrika yanatokana na jeshi kuchukua madaraka na sio raia.
Kinachoendelea ni kama Selikari wanawafundisha jeshi mbinu za kuchukua nchi. Siku ataingia General mwenye tamaa atatengeneza mapinduzi, yakifaulu anachukua nchi yakishindwa anasingizia upinzani ulitaka kuleta taharuki na kutaka kuchukua nchi.
Mungu atupe uhai wa kuyaona haya yanayopandwa leo yakiota na kuzaa matunda.
Niliwahi kuwaambia hapa kipindi kile watu wanatekwa na kupotea kwamba mbegu hii itaota na mtapata shida sana na kipindi kile aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kama sikosei alikuwa Mwingulu Nchemba alikuwa anatoa majibu simple kwamba hao watu wapo kwa wapenzi wao au ni wahamiaji haramu toka Ethiopia.
Leo yule aliyemtishia Nape bastola ambaye Waziri alisema sio askari ni mmoja wa ma askari wanaotuhumiwa kwa mauaji na Mwingulu yupo ofisini hajajiuzuru.