Ukimuacha Tundu Lissu, hivi kuna Mtanzania mwingine ameshawahi kuhudhuria kipindi cha HardTalk?

Sayansi alisoma kwa lugha gani huyo jiwe?

Si mnasema ana PhD?? Form1 mpaka 4 kasoma kiingereza, 5 na6, diploma, bachelor degree, masters, doctorate, na bado hata kujielezea sekunde 30 hawezi 😂.

Bwashee acha utani
 
Kwani BBC Hard talk ndio kipimo cha nini?
Naomba nitembelee unyayo wako mkuu. Hardtalk zaidi ya kuongea inamchango gani katika maisha yako binafsi unaehojiwa au taifa lako?

Waafrika hardtalk ina mchango gani zaidi ya kuonesha ujinga wetu kwa kudharauliana mbele ya wazungu huku wao wakiuza dharau hizo kwa hela ndefu wakati wewe hupewi hata chai ya rangi?

Mtoa mada unameona lissu wa thamani kwa sababu ya hardtalk. Baada ya hapo anakuletea huduma za jamii?

Hatuhitaji kiongozi mahiri wa kuongea, bali wa kutenda.
 
James Martin,

Mara nyingi Hardtalk inawahusu watu waliofanya vitu ambavyo vinatia shaka kwenye jamii - yaani vitu vibaya kwa jamii!
Mfano Rais Mkapa ilikuwa inahusu vifo vilivyo tokea Pemba.

Lissu alifanya vitu vya kishenzi kwa nchi yake Tanzania vilivyo wastaajabisha watu wote duniani! Kama ulielewa talk yenyewe. Hata ukimsikiliza huyu anayeulizwa sasa hivi ni kituko.

Raisi Magufuli siyo kituko, anafanya vitu vizuri hawezi akawa an interesting person for Hardtalk.
 
Sayansi alisoma kwa lugha gani huyo jiwe?

Si mnasema ana PhD?? Form1 mpaka 4 kasoma kiingereza, 5 na6, diploma, bachelor degree, masters, doctorate, na bado hata kujielezea sekunde 30 hawezi 😂.

Bwashee acha utani
Bwashee unaelewa maana ya kusomea lugha.... Ni wale wa HGL, KLF nk nk!
 
Kuwa kwenye Hard Talk , hakumaanishi wewe ni bora zaidi, ni kwa sababu kwa wakati huo una umaarufu wa muda kwa newsmakers.
Kupigwa risasi 16 kwa mwanasiasa, tena wa upinzani, lazima litamletea umaarufu as a News Item.

Kuna watu wa kila aina wanao hojiwa HardTalk, wengine kwa mabaya waliyoyafanya au walitofanyiwa. Hata Hitler angekuwa hai leo , hardtalk wangemtaka kumuuliza maswali.

Inasikitisha sisi waTZ, kwa umbumbumbu wetu tunaina ni fahari kuwamubashara kwenye vipindi ambapo mtu anahojiwa na mzungu.
 

Hao wote uliowataja bado sijawaona wakikalia kiti cha moto kama Hardtalk kwahiyo naona akili ya Lisu iko sharp kuliko wao. Nataka niwaone wakijaribiwa na waandishi wa ki kweli kweli.
 
Wataenda vipi kama mwenyekiti mwenyewe ngeli ni ya kulenga kwa mitama ya mchomvu,

"Wi a in ze raiti traiki"
Acha kabisa, hapo hata Shakur angemhoji yeye ndio angetoka mbio

Your browser is not able to display this video.
 
Nyalandu akiwa Waziri wa Maliasili 2014 alikaa uso kwa uso na Stephen Sackur kwenye Hard Talk. Jamaa Nyalandu ana English imenyooka safi na by then nilikuwa nje ya Tz kwa ngeli yake jamaa aliniinua sana mbele ya wale wenyeji wa nchi ile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…