Kila nikimwangalia mtoto mchanga huwa napata picha fulani ya Kiungu. Ni picha ya ajabu. Mfano, nikimwona mtoto ana mzazi au mlezi wake huwa napenda kuona ana'behave' namna gani.
Unaweza kumwona mtoto mchanga amebebwa na mama yake na amelala usingizi na hana habari ya kinachoendelea karibu naye. Wakati mwingine inaweza kutokea nyumbani kuna shida fulani na mnaulizana (baba na mama) namna ya kuitatua na mtoto au watoto wao hawana habari kabisa - wanaonyesha kufurahi na kuendelea kucheza.
Picha ambayo huwa inanijia ni ile ya Mwenyezi Mungu anavyotutunza na sisi tunajisikia salama na tukipata shida tunamkimbilia kwa sababu tunajisikia anatulinda kwa kuwa karibu naye, sawa na mtoto akiona kitu cha kuogopesha anamkimbilia mzazi/mlezi au ndugu aliye naye. Hivyo, ndivyo pia tunavyojisikia salama tukiwa mikononi mwa Mwenyezi Mungu.
Leo mtoto wangu alikuwa anataka chai anywe na kwa vile ilikuwa ya moto, ilibidi niipoze kwanza kabla ya kumpa. Yeye aliona nakataa kumpa, hivyo alilia na kujiviringisha chini. In the meantime, nilimaliza kuipoza nikampa. Akaanza kunywa na kutabasamu (na alionekana ameshasahau kwamba alikuwa akilia na kuniona kama nimemnyima chai).
Kwa kitendo hicho, nilifikiria kwamba, wakati mwingine tunataka au tunamwomba Mwenyezi Mungu kitu ambacho kwa uelewa wetu tunaona kinatufaa kwa wakati huo,
Lakini mbele ya Mwenyezi Mungu sivyo na ndiyo maana tunaweza kuomba na tunaona kama Mungu hatusikii au amepuuza sala zetu, kumbe kama ilivyo tokea kwa mtoto wangu, 'bado anapoza chai na akiona imepoa' anatupa na ndio wakati wa kufurahi na kusahau mateso yetu.
Je, wewe huwa unapaata picha gani?