UKIMWI (AIDS) sio ugonjwa, bali ni mkusanyiko wa magonjwa, na yote yanatiba zinazofahamika, Kuna mtu anabisha?

Duh, Ukimwi umefikia kiwango cha kudharauliwa kiasi hiki? Hebu bwana Trump sitisha ruzuku ya ARV heshima irudi.
 
Una IQ ndogo halafu husomi kwa makini, hizo organ failure si nimesema ni madhara ya kutumia ARV? Au hujui kusoma?
Sasa wewe mwenye IQ kubwa ninini kilisababisha huyo ndugu kupatwa na ukichaa kabla ya kuanza kutumia hizo ARV?
 
Likiwa moja moja yanatibika ila kwa mkupuo ngumu sana mkuu. Mashambulizi yanakuwa makali mno na kinga za mwili zinaelemewa
Mhhh! Mbona Myahudi aliweza kuyamudu yale mashambulizi ya mkupuo (axis of war)? Sema tu kuna kitu bado hakijawekwa sawa. Ni kweli ni Mradi wa watu au ni kweli ni Mkakati wa watu au ni kweli ni Uganjwa? Ugonjwa halafu miaka yote bado Tiba haijapatikana. Cjui.
 
Trump kapress kidogo tu huku pamejipa, tuungane tu tendo lifutwe hilo lina majanga sana.
Lile tendo liliwekwa kwa ajili kuzaa watoto halafu raha by the way tu... shida watu (hasa hasa weusi na masikini) tumeamua kulifanya tendo lile kama starehe na pia kama lifetime achievement goal
 

mtu mwenye immunity ndogo hata ukimuweka kwenye sterile environment,
Bado kuna normal microbiomes watamshambulia.
Lakini pia kuna cancers cells.
Hivi vyote immunity inapokuwa imara huwa inadhibiti.
 
mtu mwenye immunity ndogo hata ukimuweka kwenye sterile environment,
Bado kuna normal microbiomes watamshambulia.
Lakini pia kuna cancers cells.
Hivi vyote immunity inapokuwa imara huwa inadhibiti.
Microbiomes watoke wapi wakati ni ‘hypothetically’ absolute sterile environment?
 
 
Wewe uliwaona wapi ukiacha kwenye TV? Walikuonyesha wakichotaka uone.., hata sasa wakitaka watakuonyesha tena endapo mngegomea kama walivyogoma SA..
Duh!!! Wewe utakuwa dogo wa miaka ya 1990s imekuja kuwa na akili umekuta watu wanatumia ARVs kwa hiyo hawakondi na kuugua mpaka kufa kama ilivyokuwa kwa watu wenye HIV/AIDS wa miaka ya 1985 mpaka ARV zilipoanza.
 
Duh, Ukimwi umefikia kiwango cha kudharauliwa kiasi hiki? Hebu bwana Trump sitisha ruzuku ya ARV heshima irudi.
Mimi nawashangaa hawa watoto waliozaliwa kuanzia miaka ya 1990s hawakuwahi kuona watu walivyokuwa wanaugua huu ugonjwa kabla ya ARV kuanza!!!! Wanadanganyana kweli na kubeza!!!!
 
Haya sasa kumekucha [kwa sauti ya mzee majuto], kumbe akili mnazo hamtaki tu kuzitumia.
 
Mkuu mimi siyo daktari ila kwa kusoma soma ninaona unachozungumza hapa kina utofauti wake.

Kwanza Ukimwi ni ukosefu wa kifa mwilini kama ulivyosema. Na ni kweli kila binadamu at some pointi n life huwa anapitia hiki kipindi kinaweza kusababishwa na ukosefu wa mlo mzuri, depression, tiba kama vile chemotherapy na kadhalika. Hizi ni rahisi kuwa reversed kwa sababu ukiondoa chanzo chake basi ni rahisi kinga kurejea kwa kiasi kikubwa katika ukawaida wake.

Lakini sasa ukosefu wa kinga mwilini unaosababishwa na kirusi cha HIV, hii inaleta utata kwa sababu kirusi kinashambulia seli ambazo ni muhimu katika kukupatia kinga hii.

Na kumbuka, mwili wako mara zote unapambana na magonjwa kwa kushambulia bakteria, virusi n.k wakati mwingine wewe bila hata kujua kwa sababu upati effects wala dalili za magonjwa hayo na mwili unamalizana nayo juu kwa juu.

Sasa unapokuwa na kirusi kinachoshambulia kinga yako ya mwili, ina maana chanzo cha kufanya kinga yako ya mwili irudi si kula tu mlo wenye viini lishe maana bado seli za kinga mwili zitashambuliwa hata zikizalishwa. Kumbuka virusi hivi vinaingia ndani ya CD4 cell.

Hii ni tofauti na hali zingine zozote zinazokupatia ukosefu wa kinga mwilini ambapo mlo kamili na mfano kama watumia chemotherapy ukaacha basi inaweza kupanda pasipo kushambuliwa na chochote.

Hivyo, ili kuweza kupandisha kinga ya mwili lazima kuzuia kile kinachoishambulia hii kinga kiache kuishambulia na hii ndiyo maana ARV hufanya kazi kwa kuzuia au kupunguza kuongezeka kwa virusi vya HIV kwenye damu ili kupunguza mashambulizi ya kinga mwili.

Kumbuka mkuu kuwa, hutumiaa dawa kila mara kwa sababu una kinga mwili iliyo thabiti. Na kuna dawa nyingi tu unazitumia kazi yake wala haziui bakteria wala virusi, bali zinakupa nafuu huku kinga mwili ikishughulika navyo yenyewe.

Kuna sehemu umesema kuwa je hakuna njia nyingine ya kuongeza kinga mwili?

Nadhani hadi hivi sasa dawa zilizothibitishwa za kupambana na HIV hakuna hata moja ambayo inua na kuonda kabisa virusi hivyo kwenye damu ndiyo maana unakuta mtumiaji anaendelea tu kutumia dawa kwa kipindi chote.

Na matumizi ya dawa si ARVs tu hata ingekuwa tunatumia dawa za malaria indefinitely bila shaka figo zetu zineathiriwa. Sasa hapa ni kuchagua kutumia ARVs uishi kwa kipindi kirefu zaidi ila uje kufa kwa figo kufail au uache ufe mapema kwa magonjwa nyemelezi.

Until chanzo ambacho ni HIV kimeweza kushughulikiwa na kuondolewa kabisa, bado ARV itaendelea kuwa ndiyo solution.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…