robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 762
- 1,236
Nahisi viongozi wetu wana usahaulifu au uelewa usiolingana na wananchi wa nchi hii. Viongozi wa dini wamepinga matumizi ya kondomu miaka yote, lakini hatujawahi sikia serikali ikiagiza wakamatwe. Dini zote kubwa hapa nchini, hawataki kuruhusu waumini wao kutumia kondomu. Kosa la Gwajima lina tofauti gani na hao wengine?
UKIMWI unaua watu wengi Afrika hii na Tanzania yetu kuliko COVID-19. Kinga ikiwa ni matumizi ya kondomu. Kondomu zikapigwa vita hadhalani! Serikali hawa hawa! CCM hawa hawa! Hadi leo wameufyata! Nauliza swali kama la Gwajima, Chanjo ina manufaa gani kwa viongozi wetu kuliko barakoa?