UKIMWI upo ndugu zangu

UKIMWI upo ndugu zangu

Washkaji walimtonya demu anaukimwi
Wakat nipo udsm 2014 namaliza chuo..kuna wana wawil walikuwa ni viwembe balaa..wote wanatokea moshi,..hao walikua wanahadithia kabisa jinsi wanavyowala mademu ambiance na ma baa medi..na wao ni kutwa kushinda sinza na survey na mabaa ya mwenge pale.kitimoto kwa sana na gambe...kuna mmoja nilianza ona afya yake ina dorora nkasema tayar,nilikua nimewapita darasa moja.

2017 nikaskia mmoja kadanja,then 2018 nkaskia mwingne nae kadanja..nkasema
Kwel watu wanapotea aisee
 
Kwani kupata hiv kuna ujanja au ushamba mkuu? Ngoma anapata yoyote, awe mwaminifu anakutana na asiye mwaminifu...anapata.

Huwezi kutumia kinga kila mara, huwezi kuwa unapima kila mara.

Hakuna mwenye guarantee ya kutopata huu ugonjwa.
Hili ndio tatizo la waafrika, huku ulaya kondom kwenye kumbato ni kama jembe kwenye kulima. Yaani hakuna demu utambato kavu labda mkubaliane kupata watoto na kuanzisha familia.
 
UKIMWI upo ndugu zangu , nimetoka kumpeleka rafiki yangu hospital kupima ukimwi
ameathirika aisee , analia mpaka basi, amekata tamaa.

Tuwe makini na wadada.
Mpe ushauri maisha yanaendelea. Ukimwi wa sasa umepungua nguvu hivyo ataishi miaka mingi tu akifuata ushauri wa madaktari.
 
Shida sio utakufa lini. Ni ule uhakika kwamba muda wowote unaweza kufa.

Ukimwi ni death sentensi hata kama hutakufa kesho
Si kweli kabisa mkuu, unaweza ishi vizuri kabisa tena bila ya changamoto zozote za kiafya hata kwa miaka 40 mbele. Kuna watu nawajua walipima tangu miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni, mpaka leo wako poa na hawaifichi hali yao ingawa kunyanyapaliwa bado kupo sana. Tatizo ukiamua kujificha, hautumii dawa ipasavyo, lishe duni n.k lazima uondoke mapema.
 
Akitulia Kama hatojali akupe namba za huyo demu anayemuhisi ana Ukosefu Wa Kinga Mwilini,,nawe nipasie Mimi na shida nae mnoo
 
Poleni vijana..hyo ni ajali kama ajali zingine..unaweza kuta kuna malaya wa muda wote ila haupati ila jaribu ww sasa.....yani wengine hatukupima mpk tumepata mimba za kwanza ndo tukapimwa humo humo kilazima na kujua kumbe kikombe kilituepuka....ila hii kwenda kupima kwa hiyari inahitaji moyo...
 
Wakuu nina swali kidogo: Hivi mtu anaweza kuishi na VVU/UKIMWI hata miaka 5 au zaidi na asione dalili zozote?
 
Back
Top Bottom