Ukimya wa Freeman Mbowe kwa haya yanayoendelea unatisha sana

Mbowe hana jipya na wala hawezi kusaidia katika mapambano haya, huyo alikuwa tapeli la siasa mtu wa ccm aliyefanikiwa kulaghai wtz. Hafai hata kidogo na akae pembeni KABISA.
Tulimwambia vijana wake enzi hizo hawakusadiki tena na matusi juu ila muda umekuwa mwalimu
 
Acha mzee apumzike. Ni zamu ya Lissu acha atubebee msaraba.
 
Nani amewadanganya kuwa matusi ni demokrasia? Ni kweli amekuwa mfano wa kuigwa kwa kukubali kushindwa na kumpisha aliyemshinda bila kushurutishwa. Lakini hata hiyo hamkuridhika maana mmeendelea kumtusi, kumsimanga na kubeza kila kitu alichofanyia Chadema. Mbaya zaidi mkawaandama wale wote walioonyesha wazi kuwa bado wanamheshimu.

Heche alimuambia " tunakuheshimu sana lakini sasa huu ni wakati wa kuwaachia vijana wako wakuthibitishie kuwa tumekomaa". Basi muonyesheni.

Amandla...
 
Mwacheni mzee wa watu afanye maisha yake,Chadema mlimsema mpaka basi,nafikiri sasa hivi hata afya yake imeimarika maana hajihusishi tena na kero za CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…