Ukimya wa Katiba ya JMT Kuhusu Kifo cha Mgombea Urais

Mada Fikirishi

Katiba yetu inaongelea kifo cha Rais akiwa madarakani lakini haiongelei Mgombea Urais ambaye tayari ni Rais akifa akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu. Natoa mfano ili uelewe kwa urahisi kwamba JPM angekufa akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu Katiba haisemi kitu gani kifanyike zaidi tu ya kusema nafasi ya Rais itachukuliwa na Makamu wa Rais. Sasa yafuatayo hayana majibu ya Katiba:-

1. Je, kama Mgeombea Urais akifa kwenye kampeni za uchaguzi nafasi yake itajazwaje?

2. Je, Makamu wa Rais anayerithi kiti cha Rais ndiye atakuwa Mgombea nafasi ya Urais?

3. Je, atateuliwa mwingine na chama kujaza nafasi ya Mgombea Urais? Au atajaza nafasi ya Makamu wa Rais kwa kuwa Makamu wa Rais aliyekuwepo tayari amerithi kiti cha Rais na kuwa Rais?

4. Kama Makamu anayerithi kiti cha Rais siyo strong kushinda uchaguzi yaani siyo kipenzi cha wapiga kura wengi na kwamba akipewa kurithi pia nafasi ya Mgombea Urais aliyekufa kwenye kampeni huenda chama kikapoteza ushindi je, hapa chama au serikali iliyoko madarakani itamshusha Rais huyu (ambaye alikuwa Makamu zamani) toka kwenye kiti cha Rais ili arudi aendelee kugombea nafasi yake ile ile ya awali ya Makamu wa Rais aliyokuwa akigombea kabla Mgombea Urais (ambaye alikuwa Rais) kufa wakati wa kampeni za uchaguzi?

5. Je, hiyo siyo demotion/kushushwa cheo kwa Rais?

6. Je, Katiba inatoa maelekezo yoyote kuhusu demotion ya Rais toka kuwa Rais na kurudi kuwa Makamu wa Rais?

7. Japokuwa iko wenye Katiba kuhusu kifo cha Rais akiwa madarakani lakini kama taifa hatukujiandaa na kifo cha Rais akiwa madarakani, ni vivyo hivyo kumbe kwamba hata sasa kama taifa hatujajiandaa na kifo cha Rais ambaye ni Mgombea nafasi ya Urais; kwenye kampeni za uchaguzi mkuu. Kipi kifanyike? Au tuige Katiba ya Urusi ambayo Rais anaweza kuondoka Ikulu na akawa Waziri Mkuu na kurudi kuwa tena Rais Ikulu?
Mkuu, naomba nikusaidie maana unachanganya mambo mawili. Mambo unayochanganya moja linahusu kumpata Rais endapo Rais amefariki, pili ni kumpata mgombea wa kiti cha Rais endapo mgombea amefariki wakati wa Kampeni.

Ikiwa Rais mfano Magufuri angefariki wakati wa Kampeni ( wakati wa kugombea muhala wake wa pili) ,yafuatayo yangefanyika. Kwa kuwa kiti cha Rais kingebaki wazi utaratibu wa kujaza nafasi ya Rais ungefanyika yahani makamu wa Rais angeapishwa kuwa Rais wa nchi.

Pili,kwa kuwa chama cha mapinduzi (CCM) kingekuwa kimepoteza mgombea sharia ya uchaguzi inataka chama kilichopoteza mgombea kujaza ( kuteua) mgombea ndani ya wiki mbili,alafu mchakato wa uchaguzi ungeendelea.

Kutokana na utaratibu huo, ingebaki utashi wa CCM kuamua kama Samia S.Hassan ateuliwe kuwa mgombea au wateue mwingine. Hivyo katiba katika hilo haijanyamaza, tatizo ni wewe na watu wa aina yako kutokutofautisha mambo ya serikali na yale ya CCM kama chama.

Baada ya ufafanuzi huu wa chumla nitakuwa najibu hoja zako mojamoja.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mkuu sheria ya uchaguzi imetoa maelekazo ya hili. Ikitokea mgombea wa urais au Makamu kufariki tume ya uchaguzi itatoa nafasi kwa chama kuteua mgombea mwingine ndani ya wiki mbili na tarehe ya uchaguzi kutangazwa
Nakubaliana nawe Mkuu kwa 100% ila what if marehemu alikuwa ndiye Rais kwa wakati aliokuwa akifa kwenye kampeni? Tafakari yafuatayo:

4. Kama Makamu anayerithi kiti cha Rais siyo strong kushinda uchaguzi yaani siyo kipenzi cha wapiga kura wengi na kwamba akipewa kurithi pia nafasi ya Mgombea Urais aliyekufa kwenye kampeni huenda chama kikapoteza ushindi je, hapa chama au serikali iliyoko madarakani itamshusha Rais huyu (ambaye alikuwa Makamu zamani) toka kwenye kiti cha Rais ili arudi aendelee kugombea nafasi yake ile ile ya awali ya Makamu wa Rais aliyokuwa akigombea kabla Mgombea Urais (ambaye alikuwa Rais) kufa wakati wa kampeni za uchaguzi?

5. Je, hiyo siyo demotion/kushushwa cheo kwa Rais?

6. Je, Katiba inatoa maelekezo yoyote kuhusu demotion ya Rais toka kuwa Rais na kurudi kuwa Makamu wa Rais?
 
Dah Dogo hivi viporo vya kande iliyochacha unavyofakamia na kuparamia hadi kuvimbiwa vina kufanya unaota ukiwa umelala hapo sofani sebuleni kwa shemeji yako ukidhani huko ofisini.

Sasa sicheki ni amri amka mara moja ukachakarike vibaruani huko.
😂😂😂😂😂😂we kalili hivyo hivyo.
 
Kanda ya Ziwa ina Majimbo 42, ni Mika gani inayoiita kanda ya Ziwa? Geita tu ina majimbo 7, kagera, mwanza, Mara, shinyanga, simiyu, katavi, kigoma, tabora.
Kigoma na Tabora ziko Kanda ya Magharibi.
Kanda ya Ziwa na idadi ya Majimbo yake:-
1. Mara - 7
2. Mwanza - 7
3. Geita - 6
4. Kagera - 9
5. Shinyanga - 6
6. Simiyu - 7
 
Dah Dogo hivi viporo vya kande iliyochacha unavyofakamia na kuparamia hadi kuvimbiwa vina kufanya unaota ukiwa umelala hapo sofani sebuleni kwa shemeji yako ukidhani huko ofisini.

Sasa sicheki ni amri amka mara moja ukachakarike vibaruani huko.
Mbona nawe unamuunga mkono, unasema ......ukidhani huko ofisini... yaani yuko ofisini.
Labda ungesema .....ukidhani uko ofisini, hapa ni kwamba hayuko ofisini.
Watanzania tunangoza kwa kukijua kiswahili!
 
Hamna mada fikirishi hapa ni uvivu tu wenu wa kutafuta maarifa....mgombea urais akifariki kwenye kampeni zoezi zima linaitishwa upya Chama kitatakiwa kuteua mtu ambaye atakuja na mwenza wake.
Revise message of the post.

Nimeuliza Mgombea Urais ambaye ni Rais kamili wakati anagombea. Nikatoa mfano wa JPM angekufa kwenye kampeni. Baghosha!

4. Kama Makamu anayerithi kiti cha Rais siyo strong kushinda uchaguzi yaani siyo kipenzi cha wapiga kura wengi na kwamba akipewa kurithi pia nafasi ya Mgombea Urais aliyekufa kwenye kampeni huenda chama kikapoteza ushindi je, hapa chama au serikali iliyoko madarakani itamshusha Rais huyu (ambaye alikuwa Makamu zamani) toka kwenye kiti cha Rais ili arudi aendelee kugombea nafasi yake ile ile ya awali ya Makamu wa Rais aliyokuwa akigombea kabla Mgombea Urais (ambaye alikuwa Rais) kufa wakati wa kampeni za uchaguzi?

5. Je, hiyo siyo demotion/kushushwa cheo kwa Rais?

6. Je, Katiba inatoa maelekezo yoyote kuhusu demotion ya Rais toka kuwa Rais na kurudi kuwa Makamu wa Rais?

Mtafuta maarifa anakuwaje mvivu?
 
Kigoma na Tabora ziko Kanda ya Magharibi.
Kanda ya Ziwa na idadi ya Majimbo yake:-
1. Mara - 7
2. Mwanza - 7
3. Geita - 6
4. Kagera - 9
5. Shinyanga - 6
6. Simiyu - 7
Kigoma na Tabora ni Wale wale mkuu pili dar imetawaliwa na ukanda huo huo
 
Kitendo cha Samia kuchukua Urais bila watu kutarajia kama ingetokea kimeleta makasiliko makubwa kwa baadhi ya watu, ni kama hawakubali lakini wanashindwa wafanye nini.
 
Kuna madhara zaidi ya ikulu kuongozwa na kikundi cha wastaafu wahuni waumini wa freemasaon? Hakuna anaeogopa mgawanyiko kwa sasa kilichobaki kila mtu ale kipande chake jiandaeni kwa tanuri mnaobeza kanda ya ziwa mjipange wakati ukifika na tujimbo twenu twa vipepeo. Tungoje wakati
Criminal!

Mimi niko Kanda ya Ziwa lakini sioni na siamini katika mantiki ya fitina za Ukanda.
 
Kitendo cha Samia kuchukua Urais bila watu kutarajia kama ingetokea kimeleta makasiliko makubwa kwa baadhi ya watu, ni kama hawakubali lakini wanashindwa wafanye nini.

46E48A15-8E2A-43C8-AEE2-C876965BBFB3.jpeg
 
Mada Fikirishi

2. Je, Makamu wa Rais anayerithi kiti cha Rais ndiye atakuwa Mgombea nafasi ya Urais?
Hilo si suala katiba,itabaki utashi wa chama husika,mfano CCM wangeamua mgombea awe Mama Samia ( ambaye angekuwa ameapishwa tayari kuwa Rais) au wangeweza kuteua mwingine.Ili mradi sheria ya uchaguzi inawataka wateue mgombea mwingine baada ya kifo cha mgombea wao.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Crimial!

Mimi niko Kanda ya Ziwa lakini sioni na siamini katika mantiki ya fitina za Ukanda.
Kama mzindakaya kafa basi na mengineyo yanakuja, moto huzimwa kwa moto. Chapa kazi na kazi iendelee mtajua kuua na kuuliwa vyote ni lugha hasi.
 
Mkuu kweli mada fikirishi!japo naona kama mpango wa kukatisha ndoto za hangaya 2025 ukawepo kwa wenye kinyongo cha kuondokewa na mpendwa wao!!kuna uzi humu uliletwa eti kanda ile italipa kisasi japo hatujui watalipa kwa nani!!!!!Labda ndio maana ulinzi wa hangaya umeimarishwa????!!!na hangaya kesha anza rasmi kampeni kule Arusha!!!!
Tanzania hakuna siasa za ukabila na ukanda, watu wanalazimisha humu mitandaoni lakini katika hali halisia hakuna kitu cha namna hiyo, tunaishi kwenye jamii na hatuoni vitu hivyo ingawa humu mitandaoni mnaipigia chapuo sana

Siasa zetu zinaongozwa na upenzi, ushabiki na unazi wa vyama tu, aliye chadema hata kama mgombea wao ni mbovu kiasi gani katu hawezi kupigia chama kingine, vivyo hivyo na kwengine, mtu wa ccm hawezi kabisa kupigia chama kingine hata kama mtu aliyepo upande wake ni mbovu na hatoshi
Wachache wanaobaki ndio hupima kuona ubora wa mtu

Kama watu wakipiga kampeni za kikanda na kikabila hakika Kanda ya ziwa hamuwawezi, lakini kwa nini ifikie huko?

Hili jambo la kupandikiza chuki kwa jamii na kuwananga watu kila kukicha wanasiasa wanaweza litumia kama mtaji na mwisho wa siku twaweza jikuta katika siasa za ukabila na ukanda

Hivi Mark na Dr walipigwa jungu zipi? Zilikuwa za kikanda?
Kamati zikishaamua wengine ni wapiga miluzi tu

Elimu ya siasa Tanzania ni ndogo
 
Ndiyo miongoni mwa hao ninaosema wamekerwa lakini hawajui wafanyeje wamebaki kuzua maneno tu ila wakae wakijua wanaye hadi 2030.
Inatakiwa itengenezwe katiba isiyotoa mwanya kwa mtu kujipatia madaraka kama mtu anayeokota embe dodo kwenye mti wa mbilimbi,CCM wajue katiba bora ni yenye maslahi kwa wananchi wote wasifikirie kulinda madaraka yao tu.
 
Nakubaliana nawe Mkuu kwa 100% ila what if marehemu alikuwa ndiye Rais kwa wakati aliokuwa akifa kwenye kampeni? Tafakari yafuatayo:

4. Kama Makamu anayerithi kiti cha Rais siyo strong kushinda uchaguzi yaani siyo kipenzi cha wapiga kura wengi na kwamba akipewa kurithi pia nafasi ya Mgombea Urais aliyekufa kwenye kampeni huenda chama kikapoteza ushindi je, hapa chama au serikali iliyoko madarakani itamshusha Rais huyu (ambaye alikuwa Makamu zamani) toka kwenye kiti cha Rais ili arudi aendelee kugombea nafasi yake ile ile ya awali ya Makamu wa Rais aliyokuwa akigombea kabla Mgombea Urais (ambaye alikuwa Rais) kufa wakati wa kampeni za uchaguzi?

5. Je, hiyo siyo demotion/kushushwa cheo kwa Rais?

6. Je, Katiba inatoa maelekezo yoyote kuhusu demotion ya Rais toka kuwa Rais na kurudi kuwa Makamu wa Rais?
Katiba inaelekeza/ndiyo iliyoweka hiyo demotion kwani imesema huyo Rais ambaye alikuwa Makamu kabla kifo cha Rais, kwamba ANAWEZA kuteuliwa kugombea.
 
Kitendo cha Samia kuchukua Urais bila watu kutarajia kama ingetokea kimeleta makasiliko makubwa kwa baadhi ya watu, ni kama hawakubali lakini wanashindwa wafanye nini.
Kwa sasa naamini 100000000000% mamlaka ya kutawala na RIZIKI yanatoka kwa MWENYEZI MUNGU na sio kwa KIUMBE chochote kile (vitabu vyake vinasema, aliyepandishwa juu na M/MUNGU hakuna awezaye kumshusha na aliye shushwa na M/MUNGU hakuna awezaye kumpandisha).
 
Crimial!

Mimi niko Kanda ya Ziwa lakini sioni na siamini katika mantiki ya fitina za Ukanda.
Katika siasa lazima kama chama muwe na uhakika wa uungwaji mkono katika maeneo kadhaa ambayo ni ngome yenu,
ambayo huwa mnaungwa mkono wakati wote na mnaushawishi na maeneo hayo usio na shaka.
Kanda ya ziwa kwa kiasi kikubwa ilikuwa ngome ya ccm ukitoa jimbo la cheyo,
Ndio maana haikuwa rahisi 2010 nyamagana na ilemela kutangazwa majimbo ya chadema.
kama ambavyo kaskazini ni ngome ya chadema.
Kuingiza kanda ya ziwa katika maeneo yasiyotabilika kama yatapigia ccm au upinzani
ni kuitoa kanda ya ziwa katika maeneo ambayo ni ngome mhimu kwa ccm.
 
Mada Fikirishi

3. Je, atateuliwa mwingine na chama kujaza nafasi ya Mgombea Urais? Au atajaza nafasi ya Makamu wa Rais kwa kuwa Makamu wa Rais aliyekuwepo tayari amerithi kiti cha Rais na kuwa Rais?
Makamu wa Rais angekula kiapo kuwa Rais, baada ya hapo kwa kushauriana na chama chake angemteua makamu wa Rais.

Chama cha mgombea aliyefariki ambaye pia alikuwa Rais,kingependekeza mgombea mwingine wa kiti cha Urais. Kwa utashi wa chama husika wangeweza kumpendekeza Rais aliyekula kiapo ( yahani aliyekuwa makamu wa Rais) ama wangependekeza jina la mwanachama mwingine kuwa mgombea wao.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mada Fikirishi

4. Kama Makamu anayerithi kiti cha Rais siyo strong kushinda uchaguzi yaani siyo kipenzi cha wapiga kura wengi na kwamba akipewa kurithi pia nafasi ya Mgombea Urais aliyekufa kwenye kampeni huenda chama kikapoteza ushindi je, hapa chama au serikali iliyoko madarakani itamshusha Rais huyu (ambaye alikuwa Makamu zamani) toka kwenye kiti cha Rais ili arudi aendelee kugombea nafasi yake ile ile ya awali ya Makamu wa Rais aliyokuwa akigombea kabla Mgombea Urais (ambaye alikuwa Rais) kufa wakati wa kampeni za uchaguzi?
Hili litabaki utashi wa chama na mgombea wanayemtaka wao. Wanaweza kuamua kumpendekeza Rais aliyerithi kiti cha Urais kilichoachwa wazi au kumpendekeza mwanachama Mwingine.Katiba yetu haijamzuia Mtu yeyote aliyewahi kuwa rais, kushikilia Wadhifa au nyadhifa zingine. Imeweka ukomo tu wa kuwa Rais Kwa muda husiozidi mihula miwili ya miaka mitano Kitano.Ndiyo maana tuna marais wastaafu anbao ni wakuu wa vyuo.

Back
Top Bottom