Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kila jambo lina uwili...Hata kulia kuna uwili wake. .huwezi kulia milele kuna siku utacheka na huwezi kucheka milele kuna siku Italia
Sakata la usalama wa chanjo ya korona linaingia wiki ya tatu sasa kama si nne! Ni kinara wa hili sakata ni mchungaji Josephat Gwajima.
Ambaye ameshiriki kikamilifu kukwamisha, kuyumbisha na kupotosha dhana nzima ya chanjo husika! Gwajima ni kiongozi wa kiimani mwenye wafuasi wengi.. Hivyo kampeni take imeleta madhara makubaa nchi nzima.
Upotoshaji wake ambao naweza kuupa vipengele vya seasons ni kama wiki hii unaingia season four sasa.. Seasons hizi huwa zinaanza siku ya ibada Jumapili kwenye kanisa lake na huwaandaa watu kuanzia Jumatano yake!
Huko ibada zake maranyingi si za kiroho bali za kupambana na wale wote wanaoenda naye kinyume.. Huko atakuchamba, kukusiliba na kukusema atakavyo na waumini wake watashangilia sana halafu watatoa sadaka.
Je Gwajima anaijua vema miiko ya kuwa mtumishi wa kiimani? Je Gwajima anaijua vema miiko ya kuwa mtumishi wa kisiasa? Weledi? Heshima? Hekima? Tafakuri!? Utu? Katika nafasi zote mbili?
Ni wazi Gwajima kashindwa kuyatambua mambo muhimu makubwa matatu yanayomfanya awe na uono kimo cha mbilikimo.
Kashindwa kabisa kujitambua yeye ni nani Kashindwa kabisa kujjijua yuko wapi, Kashindwa kabisa kujijua anafanya nini.
Kama kiongozi wa kiimani na kisiasa kuna code of conduct inamuongoza kwenye kila nafasi! Alikuwa na nafasi nzuri kabisa ya kuwakilisha hoja Zane kupitia channel sahihi kama mbunge na pia kama kiongozi wa kiimani.
Cha ajabu kashindwa kufanya hivyo na kuamua kutumia mimbari anayoita ya kimungu kupayuka na kuropoka, yaliyokosa, weledi, yaliyokosa uhalisia, yaliyokosa ithibati, yaliyokosa heshima na hekima na yaliyojaa upotoshaji mkubwa.
Hao waumini anaowatetea wasichanjwe ukiwaona wanatia huruma..wana shida. Wana dhiki kama zote! Wamepigika kimaisha na wengi wao ni wagonjwa wa magonjwa mengine mbalimbali.
Wanatumia dawa nyingine za mzungu
Wamepata chanjo nyinginezo
Wameshawahi kupata chanjo na dawa nyinginezo na zikawaletea side effects. Wanatumia vitu vingi sub standards vyenye madhara kiafya kuanzia vyakula mpaka vinywaji na vingine vipo hapo nje tu ya kanisa lake
Sijawahi kusikia akitoa elimu ya afya kuhusiasa na vyakula vya kusindika viwandani, mbolea zenye kemikali, wanyama wa kukuzwa kwa madawa, carbonated juices, vidonge vya uzazi wa mpango na njia za kuzuia mimba zenye madhara mengi kiafya...lakini la chanjo yeye ndio kawa daktari na mshauri bingwa..
Chokochoko zake zimeingia hatua mbaya ya sasa, kutoka kisiasa mpaka mambo binafsi, mambo ya kifamilia, siri za familia ...hapa kavuka mipaka.. Ni wazi kabisa kashindwa kujitambua yeye ni nani yuko wapi na anafanya nini.
Kama ni kukosea walikosea wanasiasa na mawaziri wote enzi za kayafa... Ule utawala ulikuwa wa one man show huwezi kupingana naye kama unajipenda.. Waliokengeuka kauli sio Dorothy pekee ni karibia mawaziri wote kama sio wote!
Kwa ubovu wa katiba tuliyonayo waziri wa afya yuleyule wa Magufuli inabidi sasa aende na biti ya Samia.. Ni ngumu lakini hakuna namna labda ujiuzulu..wanasisa wetu wengi ni vinyonga na hatuna katiba nzuri ya kuwaongoza!
Gwajima anaumizwa na kuukosa uwaziri. Gwajima kwa kificho yuko nyuma ya kundi kubwa faidika enzi za kayafa ambalo halina furaha na mama Samia.. Ukiachana na tofauti zao kifamilia..Gwajima hampingi waziri wa afya anampinga rais kupitia msaidizi wake!
Serikali iko kimya sana kwenye hili.. Ni uamuzi mzuri na wa busara japo una madhara yake. Kutokurupuka kwenye ishu hii ya Gwajima kungefanyika kwa wengine na kwenye mengine ingepata mileage kubwa sana!
Gwajima anachokonoa sana ili ajibiwe..lakini hajibiwi.. Dorothy alijaribu lakini haraka sana akagundua kosa lake na kaamua kukaa kimya! Ukimya wa serikali dhidi ya upotoshaji na chokochoko za Gwajima ni kama kumpuuza lakini Gwajima amakinike kwakuwa ngoma ikivuma sana HUPASUKA!