Claret
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 758
- 987
Niwatakieni salamu nyingi siku ya leo.
Moja kwa moja kwenye mada. Kuanzia siku ya jana kumekuwepo na video na picha za majeruhi na waliofariki wenye majeraha yanayodhaniwa ni ya risasi na kwa taarifa za polisi wamekamata watu kadhaa kuhusiana na uchaguzi huku wakidai wametumia mabomu ya machozi kutawanya watu lakini sijasikia kuhusiana na majeraha na vifo ambavyo vimeonekana kwenye pucha zilizopigwa kwa simu binafsi.
Kwa upande wa vyombo vya habari tunavyoviamini kwa habari muhimu za kichunguzi hatusikii wakithubutu kuelezea wananchi yanayotokea.
Ukimya huu ambao hata watumiaji wa JF tunauona humu ni wa kutilia shaka na unaacha maswali mengi kama je hovi vyombo vinaweza kutuletea habari sahihi zisizo na chembechembe za woga na upendeleo.
Waandishi wa habari na vyombo vyao wanapaswa kuelewa kuwa wao ni kiunganishi kikubwa katika mambo ya msingi ya nchi na wakishaharibu uaminifu wanaopewa na watizamaji, wasikilizaji na wasomaji wa habari zao wanajiingiza katika janga kubwa.