Hapo kwenye elimu duni ya uraia patatuchelewesha sana.
Elimu hiyo inatolewa kimagumashi makusudi kabisa kuhakikisha raia hawaelimiki na kujitambua.
Majority ya raia nao, wasomi kwa wasio wasomi hawana utayari wa kujitambua au kujielimisha juu ya mambo muhimu ya kijamii kama masuala ya haki na wajibu, nguvu na mamlaka yao ya kiraia, badala yake ni kukomaa na mambo ya kipuuzi tu ndio maana ni rahisi kwa sisiem kufanya kila watakacho bila hofu yoyote.
Unawakuta wanafunzi na wahitimu wa vyuo vikuu wakijivunia walivyofeli somo la GS (General Study) kwa kupata S kule A level huku wakifaulu Maths, Physics, Chemistry nk. Ilishafikia kufanywa kama fashion kabisa, ukifaulu hilo somo kwa wanafunzi wa science kidizaini unaonekana kama mshamba fulani