Fikra potofu haswa.
Kama kuna Uchaguzi Mkuu ambao CCM inashiriki huku ikiwa na pancha nyingi kwenye uongozi, ngazi zote, ni wa mwaka huu.
Kitendo cha kumwengua January na Mpina kujiunga na upinzani kama mgombea Urais ni keti ya ushindi kwa vyama vya upinzani.
Iwapo vyama vya upinzani vikiamua kushirikiana, litakuwa anguko la CCM mithili ya KANU.
ANGALIZO: Vyama vya upinzani kusimamisha mgombea wa Urais, kila kimoja, ni moja ya udhaifu utakaompa mgombea wa CCM kupita kwa urahisi.
LAKINI: CCM ijiandae upinzani mkubwa kwenye awamu ifuatayo, ndani na nje ya bunge.