Ukinyang'anywa mtoto, unaweza kuchukua maamuzi kama haya?


No matter what? you can not take a 1yr baby from his mother and hide him. :frusty::frusty::frusty::frusty:
 

Mtu B, nakubaliana na wewe ni aibu ila sio aibu kwa akinamama tu, hata baba unayezaa mtoto bila utaratibu ni aibu pia, kinachoficha aibu ya mwanaume ni ile kutokulea/kuonekana na huyo mtoto. Tuna mifano ya wanaume walioaibika kwa kutelekezewa watoto na mwanamke waka ingia mitini, then tunaishia kuwalaumu wanawake. Nadhani sisi wanaume ndio chanzo cha mabadiliko 😛lane:
 
Ungekua umepata malezi ya heshima usingekua unaongea maneno machafu wewe ni C.R.A.P tu RIP

Maty mama, huyu bwana mdogo achana nae tu, hajui kiburi sio uungwana, hajui dunia hadaa, hajui huyu jamani. Mcheka kovu hufikiwa na jereha. Kiburi cha uzima hiki sio kizuri. Bora kunyamaza, bora kuwaombea hao unawaita Mbwa, bora bora, hatujui kesho yetu iko je?? Barikiwa baba angu.
 

Asante LD, mtukama huyu hajui maisha, kuna mtu aliambiwa aliyefikiria/mlea ni baba yake siye! at the age of 30. Tumuombee kwani hili ni kama UKIMWI kama huna sio kwamba we mjanja, na usiwacheke walionao.
 
Asante LD, mtukama huyu hajui maisha, kuna mtu aliambiwa aliyefikiria/mlea ni baba yake siye! at the age of 30. Tumuombee kwani hili ni kama UKIMWI kama huna sio kwamba we mjanja, na usiwacheke walionao.
Elia................. wish I could say something on this but I cant.............it pains alot........................cant say anything nabakia tu kusema,,,,,I wish I wish
 
Hao ndo wanaume, wengine ni wanyama hata kwa watoto wao,huwezi muiba mtoto niliembeba kwenye tumbo langu nikamzaa kwa uchungu akiwa na mwaka mmoja......................

Mimi singeenda mwenyewe,ningeenda na team ya wanaume na askari,tumchukue akaonyeshe mtoto aliko............

Huu ni unyama,eti chapa lapa,kuna wanaume waga wanafikiria na vichwa vya katikati ya miguu yao na si vya kawaida,am very sure!
 

Tena Mungu amesikia alichosema,sijategemea mtuB anaeza kusema alichosema..hivii?...ila yaishe.let me sleep.
 
hebu acha uongo,mi nna marafiki zangu wengi tu wamelelewa na mama zao mbona hawaichukii hiyo hali? Kwani kuna shida gani kama mtu hataki kuolewa na anataka mtoto akizaa! Kila mtu ana maamuzi yake bana ilimrad havunji sheria.

una uamuzi wako ndiyo, lakini uhuru wako na haki yako haipasi kuingilia haki ya mwingine. Una haki ya kuzaa kama mbwa koko wanaokutana jalalani kama hujali, lakini mtoto naye ana haki ya kuzaliwa katika mazingira ya staha. Kama wewe hutaki kujitunzia heshima, hilo ni juu yako, lakini unapoamua kuwa hata mtoto naye akose heshima hapo unamkosea haki sana.
 
Shukuru Mungu wewe uliyejikuta umezaliwa katika hali hiyo ya 'ndoa takatifu'

Namshukuru Mungu. Na ninawaasa wanawake waache tabia ya kujizalia tu watoto wasiokuwa na msimamo ambao wanakuja kujuta na kujisikia vibaya.
 
Hana cha ndoa takatifu huyu asingeumia kiasi hiki. Kazaliwa na hao mbuzi anaowaita
Kumbe basi unaelewa kuwa wanaozaliwa kama mbuzi hivi wanaumia kiasi hiki. Sasa mbona mnapenda kuwaumiza watoto wenu?
 

MwanajamiiOne naomba unielewe kuwa hapa sizungumzii watu kama wewe kwa sababu wewe mwanao ukimweleza atakuelewa kabisa kuwa hukuwa na nia ovu, atakuheshimu na kukushukuru kwa bidii yako ya kumlea licha ya ndoa yenu kuvunjika. Nazungumzia wale wanaoamua kwa makusudi kuzaa bila mume, matokeo yake hata cha kumueleza mtoto sababu ya kukosekana baba anashindwa, badala yake mtoto akiuliza mimi babangu yuko wapi anajibiwa 'kwani huli? huvai? unalala nje? sasa baba wa nini?' Hali kama hizi zinawakwaza watoto, zinawaumiza kihisia na kuwatesa sana. Nielewe hivyo mama, una uzoefu huo uliosema na mimi pia nina uzoefu wangu. Kinamama wawafikirie watoto wao kabla ya kuamua tu kuzaa
 

Nimepigia mstari hapo, ni kweli inauma sana, ndio maana nawaomba mama zetu mtufikirie, wafikirieni watoto wenu kabla hamjaamua kuzaa kwa mtindo huo. Mtoto hana kosa lolote, anajikuta katika mateso ya kihisia kutokana na uamuzi mbaya wa mamake aliyeamua kuwa ana haki ya kuwa na mtoto kama wanawake wengine, bila kuifikiria haki ya mtoto.
 
wewe yamekukuta ndio maana unahuzuni hivyo mimi nimelelewa na mama yangu tu na sijwahi kusikitika hata siku moja nakula maisha kwa kwenda mbele

Kwa hiyo kuwa 'unakula maisha kwa kwenda mbele', mateso ya watoto wengine huko waliko hayakuhusu siyo? Ndiyo ubinafsi huu ninaozungumzia.
 
wote wana makosa, wewe ulizaa na mwenzako then unaiba mtoto harafu kumbukja uchungu alioupata mwenzio wakati wa kuzaa. Naye mama katiba ndo imemfanya amchape knife maana hiyo inaruhusiwa kisheria kibinadamu noo. Sasa hapo na yule mama akipata wakili mzuri atashinda kesi patamu hapo pamoja nakuwa kamjeruhi. du kesi lini inatajwa tukafaidi?
 

hilo pia nakubaliana nawe 100%. Hapa napinga kinamama wanaodai ati ni haki yao kuzaa (hawajali atakayezaliwa atakuja kujisikia vipi na hali hiyo). Nimesoma kwenye gazeti moja kuna kinamama wanaitwa 'sperm jackers', anapanga kuzaa na mtu hata kama huyo mwanaume hakutaka kuzaa na wakishafanikiwa wanajisifu! Nawalaani sana wote hawa.
 
Wote wanampenda sana mtoto wao lakini Mshkaji (Dr.) kachemka.
 
Wanaume wajue mtoto ni wa mama siku zote. Ndio asili.

Dr amrudishe mtoto kwa mama yake, ikishindikana mama fungua kesi.
 
aripoti polisi mara moja kufungua kesi ya kumteka mtoto (kidnaping of a child).Mtoto wa chini ya miaka 7 anatakiwa atunzwe na mama labda kama kama mahakama imeamua vinginevyo.kwa vile mama ana uwezo wa kumlea nk na hakukuwa na makubaliano ya kumchukua awahi polisi fasta.vile vile aende ustawi wa jamii watamsaidia ushauri zaidi.Kama mtoto haoenekani that means ni kidnapping kwani amechukuliwa bila consnet ya mama.Huku umangani kesi kama hizo ziko nyingi sana manake wenzetu huoana kwa mikataba.
 
Wapendwa, samahani sana nilileta mada nikapata safari ya kwenda kijijini ambako hakuna netiweki ya Voda wala eateli isipokuwa tigo ambayo situmii... sasa nimerudi kuchangia na kujibu maswali yenu.

Nashukuru sana kwa michango yenu wote, nimefurahishwa sana na wadada/wamama wa Jeiefu kwa kuonyesha dhahiri how a mother can go an extra mile to defend and protect his/her child. Big up ladies

Nimesikitishwa sana na baadhi ya wachangiaji waliotoa kejeli na matusi na kufikia hatua ya kuita wamama wanaopata watoto nje ya ndoa kama mbwa... ina maana watoto wao ni vitoto vya mbwa....:crying:.... Kumbuka hata wewe utakuwa/una watoto (kama utabarikiwa/umebarikiwa), huwezi jua, siku moja anaweza kubadili jina akawa mbwa as well... usihukumu.... kipimo hicho hicho kitatumika kukuhukumu wewe....

Lakini kumbuka kwamba mtoto hachagui kuzaliwa na mzazi wa namna gani, but all in all MAMA WILL ALWAYS REMAIN TO BE MAMA... nobody can change that. Kuna watu wanabakwa na kupewa ujauzito, kuna watu wanahitaji watoto ndani ya ndoa na hawapati, yote ni mapenzi ya Mungu, lakini binadamu huwezi kumuhukumu binadamu mwenzako kwa sababu hukumuumba, hiyo ni kazi ya mungu...

Asanteni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…