Ukioa Kilimanjaro unakuwa ni sawa na umeolewa wewe, kila mwisho wa mwaka unatakiwa kwenda Moshi sherehe za mwisho wa mwaka

Wenzako wanaenda kutafuta connections za biashara wewe endelea kulia lia

Sent using Damu ya Yesu
 
Mchaga yupi? Kuna wamachame, warombo, wamarangu, wauru, wakibosho, waoldmoshi na wote hao wanalugha zao hawasikilizani kabisa. Ndugu zangu wameoa wamachame na wamarangu na bado wanaenda huko na kulala kwa wakwe! Au wewe unasema mambo ya mwaka 47?

Ndio maana nimesema "jamii nyingi za wachaga" nikimaanisha huenda sio wote. Ukiona mwanamke anabeba familia pamoja na mume kuwapeleka uchagani ujue hapo kuna mawili
1. Kuna tukio labda wameandaa kama vile ubarikio wa watoto na wamekubaliana wakafanyie huko. Wengi wanaofanya hivi hua wamewekeza kule kwa maana ya kujenga nyumba ya kufikia kipindi cha sikukuu maana hawawezi kulala kwenye nyumba ya baba mkwe.
2. Labda mwanaume mwenyewe aamue kwenda kule katika hali ya kubadilisha mazingira na kupumzika. Watu wengi hata wasio wachaga hua wanaenda kilimanjaro kipindi hiki kupumzika tu na kula bata kwani kunakuaga na "vibe" kama lote, hali ya hewa nzuri nk
3. Sikatai kwamba inawezekana kuna wanaume wanaoburuzwa kupelekwa kule bila ridhaa yao hasa pale unapokuta mama ndio ana sauti kwenye nyumba.
 
Ndoa ndoano wacha waende kutambika na wake zao, wakabadilishe mizimu
 
Sio kweli mwanamke aliyeolewa asielala kwao ni yule aliyeolewa maeneo ya jirani na kwao ila kama umeolewa mbali na hapo waweza lala hata mwezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingine vizuri ukaficha ulicho nacho kichwani, pita hivi. Unakichwa kigumu huelewi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajisema au? Kuna neno kuapa unamweleza mtu apa! Kuna neno watu hutamka apa wakati neno sahihi ni hapa (hapa mahala ni kuchafu). Nakereka na mtu kuondoa h katika baadhi ya maneno siku hizi mfano ivo baadala ya hivyo, ivi baadala ya hivi etc
 
Hayo ni mawazo yako potofu mbona mimi nimealika wafanyakazi wenzangu niko nao huku saa hivi tunakula bata ina maana nimewaoa?
 
Kwahiyo naww unahesabiwa au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
we n mchaga au upo tu uchagani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nna ndoa ya 14yrs na mtoto mzuri wa kichaga lkn sijawahi kwenda huko. Ni uamuzi binafsi na si kulazimishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…