Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 11,133
- 12,361
Nyie waganga wa jadi mnanufaika na hii theory ya uchawi.Wachawi wametajwa katika vitabu vyote vya dini kuwa wapo wachawi na watakuwepo mpaka mwisho wa dunia. Ukiamini sawa usipo amini pia sawa. Ngojea yakukute ndipo utakapo amini kuwa uchawi upo na wachawi wana nguvu za kumroga mtu yoyote yule wanaye mtaka.
Kuna mdau juzi kaleta uzi, anasema Ukristo kwa maana ya Biblia haikubali kwamba kuna uchawi, isipokuwa imeutaja uchawi kwa kutambua kuwa kuna jamii zinaamini uchawi.
Kwa mujibu wa mleta uzi, Biblia inasema kuwa kuna nguvu mbili tu..
Ya Mungu na Shetani.
Shetani anatumia malaika waasi ambao ni mapepo au majini.
Mapepo au majini hayaleti uchawi, uchawi na ushirikina ni imani za kipagani ambazo Biblia haizitambui.
Huyu mdau anaweza akawa yuko sahihi sana.
Mdau anaitwa mjanja-hajioneshi.