Ukiokota Pete yoyote Njiani Tafadhali usije Kuivaa itakuletea madhara mwilini mwako

Nyie waganga wa jadi mnanufaika na hii theory ya uchawi.

Kuna mdau juzi kaleta uzi, anasema Ukristo kwa maana ya Biblia haikubali kwamba kuna uchawi, isipokuwa imeutaja uchawi kwa kutambua kuwa kuna jamii zinaamini uchawi.

Kwa mujibu wa mleta uzi, Biblia inasema kuwa kuna nguvu mbili tu..

Ya Mungu na Shetani.

Shetani anatumia malaika waasi ambao ni mapepo au majini.

Mapepo au majini hayaleti uchawi, uchawi na ushirikina ni imani za kipagani ambazo Biblia haizitambui.

Huyu mdau anaweza akawa yuko sahihi sana.

Mdau anaitwa mjanja-hajioneshi.
 
nilishaokota cheni ya mkononi silver nikaivaa kwa kipindi kirefu sana siku moja nipo bondeni kuna mzee akanifuata akaniomba hiyo cheni nilipigwa na butwaa nikamuuliza umeipendea nini na yeye hakua na jibu akaniambia nimeiona toka kule baharini nikijiandaa kwenda kuvua nikaona nisiondoke bila kuja kukuona ....
nikamwambia kavue samaki ukirudi tutaongea vizuri nikupe akasepa akakaa karibu mwezi baharini wakati anarudi naona kavaa cheni kama yangu ila zimetofautiana michoro kwenye kile kisehemu kama ufito yake ina michoro kama mizizi yangu ina michoro kama gololi hivi basi ananimbia kaikuta kwenye nyavu akivua nilishangaa sana....

alikuja kuipoteza hajui ilipotelea wapi yangu nilikaa nayo mwishoe nikampa wife anaitinga mpka leo...
 
Mnakuza mambo kuliko uhalisia
Wakumbushe,"Enyi mlio na imani haba,japo tu mngekuwa na chembe ya imani kama mbegu ya haradani,mngekuwa na uwezo wa kuiamuru milima ihame na ikatii"Hata hizo mapete na vifananVyo havita wasumbueni๐Ÿค“
 
Umeandika mengi lakini haujaelezea lengo la wewe kwenda kwa mganga na kupokea masharti lilikuwa ni nini
 
Umeandika mengi lakini haujaelezea lengo la wewe kwenda kwa mganga na kupokea masharti lilikuwa ni nini
Kazi kuu ya nyumba za makuti ni maagano na mikataba.


Yaweza kuwa ni kwa njia ya
1. Jasho au
2. Damu

๐Ÿ‘บ๐Ÿ‘น๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ‘ฟ๐Ÿ‘ป๐Ÿ’€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ