T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Europe wameanza kupigana kabla Afrika haijijui inaitwaje. Unapata wapi nguvu za kudai eti Europe itakuwa na hali mbaya kisa vita ya nchi mbili ambayo hata sio full scale.Sana atakuwa anachapwa balaa. Hata yule jamaa ya Reuter safety officer wa russia wamepita naye kwenye hiyo hotel waliyokuwa wanakaa wameichakaza vipande vipande. Tatizo la hii vita ya russia na ukraine ni ya ki maslahi zaidi na haina uhalisia. Unajua walikuwa wanatuona sisi africa hatuna akili yaani ni wagomvi wakati wao ndiyo wanatugombanisha, ila kwa yanayoendelea nina uhakika europe haitakuwa ile ya kabla ya russia ukraine war, hali itakuwa mbaya zaidi na huko mbeleni hata umoja wa ulaya utasambaratika na wataingia vitani wao kwa wao
Europe imepigana vita zote mbili za dunia, na lazima ya tatu Europe ihusike. Miaka ya 1300 hadi 1400 humo Uingereza na Ufaransa waliwahi pigana kwa miaka 100 na hakuna nchi ya nje iliwapelekea chakula wala kuwasaidia kitu. Sisi Tanzania COVID-19 imetokea China, serikali yetu ikasimamia ugonjwa huo haupo na bado tukapewa hela tukazipokea kwa shangwe na kujenga vyoo.
Tena muda huo 100 years war imeanza Ulaya ikapata janga la Black Death ugonjwa wa tauni ukaua zaidi ya 40% ya watu wote wa Ulaya. Yote hayo yalitokea sisi Waafrika tukicheza ngoma, na bado wakaja kwetu wakakuta hatujui kusoma na kuandika.
Sasa leo hii Ulaya itikisike kisa ugomvi uchwara huu wa Ukraine na Russia. Omba uzima vita iishe uje uone tofauti ya sisi Waafrika na wazungu, Ukraine itarecover kwa msaada wa majirani wakati sisi Waafrika tupotupo.
Afrika kuna vita nyingi DRC, CAR, Sudan zote mbili, Somalia, Ethiopia na magaidi. Kote huko hakuna ambapo marais wa Afrika waliwahi kukusanyika kudai amani. Ajabu mwaka jana wakapeleka viribatumbo vyao Ukraine na Urusi kuomba vita iishe. We unaona Afrika tuko sawa kweli?