Ukiona unaenda kwenye matibabu na daktari anakuwa kama hajiamini hivi, anababaika-babaika katika kutafuta ugonjwa wako, na hata anatumia google jua kuwa upo kwenye mikono salama. Magonjwa ni mapana sana na yanaingiliana sana dalili.
Ukiona Daktari anakudiagnose fastafasta jua kuwa hafahamu magonjwa. Daktari anayefahamu magonjwa ukimwambia dalili kichwani yanamjia magonjwa na possibilitiies kedekede.
Hapo utaanza kumuona anasolve kwa 'elimination' anaingia na google kuconfirm na kuangalia mengine ya kufanana nayo.
Heshimu sana daktari ambaye ana mashakamashaka hivi. Daktari mwenye shule zaidi ndiye anayeonekana kubabaika zaidi.
Heshimu sana daktari anayetumia google. Ogopa ambaye anakutajia dawa mara tu baada ya kumwambia dalili zako.
Field ya afya/medicine ni pana saana.
Huwezi kuweka kila kitu kichwani kwako. Ni kweli kufanya reference ni kitu cha busara sana, ingawa wagonjwa wengi huona kama daktari ni mbabaifu.
Katika kujua tatizo la mgonjwa kuna hatia nyingi:
1: Historia
2: Ukaguzi/kuona na kushika
3: Mtizamo/mwelekeo wa daktari kuhusu aina ya ugonjwa.
3: Vipimo
4: Ugonjwa kubainika au hitaji la bipimo zaidi.
5: Dawa au rufaa ya vipimo zaidi au tiba ya hali ya juu zaidi.
6: Ushauri wa tiba husika
Kwa magonjwa mengi, ukimaliza namba mbili ni muhimu kuwa na uelekeo wa ni kinachomsibu mgonjwa(75%). Ingawa wakati mwingine matatizo hujulikana kwenye namba moja (kulingana na aina ya tatizo).
Hivyo kupima au kutokupima hutokana na asili ya tatizo au kama matatizo yanayofanana yanaelekea kuwepo au tatizo husika ni la lazima kuthibitishwa kwa kipimo, si lazima mtu kupimwa.
Pia, kufanya reference hutegemea na ni nini hasa mtu anakitafuta. Huwezi kumhukumu bila kujua anatafuta nini hasa na kwenye hatua gani katika zile sita.
NB: Referencing ni moja ya njia ya kupunguza errors/makosa kama aina ya dawa, dozi, athari ya dawa, muingiliano wa madhira ya dawa etc.