Ukiona Dalili hizi jua uzee ndio huo unabisha mlangoni

Mkuu ikikupendeza tuletee mada ya jinsi ya kukabiliana na upweke uzeeni.

Haina shida mkuu.
Ila kanuni au mbinu muhimu zaidi ni kuuziwa upweke wenyewe kwa sababu upweke haukabiliwi.
Upweke = Kifo
Upweke ni hatua ya awali ya mtu Kufa.

Kifanye kifo kuwa rafiki huwezi hisi upweke.

Ngoja niandike uzi wa mada hiyo
 
6. Kuanza kuona majina ya watu uliosoma nao kwenye pdf za teuzi za ikulu.
7. Kundi la vijana kunyamaza kwa heshima na kukusalimia ukipita.
8. Kuanza kusoma makala za afya na kumzingatia Profesa Janabi.
9. Kutopenda safari ndefu. Mimi kwenye 20s nilikuwa natoka Arusha na Saibaba ya mwisho naingia Dar usiku sana halafu saa 12 niko kwenye buti la Zungu kwenda Mtwara. Nikifika Mtwara naweza kuunganisha hadi Songea. Sasa hivi safari zangu lazima ziwe na maandalizi.
10. Kutopenda vyakula vya migahawani.
 
Mbona Mimi sipendi vyote hivyo Toka nikiwa mdogo? Baba alibidi aninunukie redii niende nayo Sekondari maana nilikuwa napenda mambo ya habari habari wakawa wananiita dingi 🤣🤣

Mziki jiliowahi Kucheza napo nilikuwa naenda kutafuta videmo ni vigodoro tuu japo Hadi Leo hii nimewahi ingia klabu si zaidi ya mara 10.

Kwa hiyo Mimi nilizeeka since Nina Miaka 9 Sasa 😆😆
 
Nilivyokua chuo nunua chapu PC na sub woofer,muziki mkubwa ghetto,siku hizi muziki sauti kubwa naona kero
 

Alafu hautaki gari lenye vurugu. Wakati ukiwa kijana unataka mambo yawe Yenteyente
 
Points nne umepatia lakini namba 2 umekosea...mi ni mzee wa miaka 50 lakini sikosi live band makumbusho, oldskool disko pale Ada Estate, hata pale Rotana kwa mzee Kisauji huwa sikosi...na napenda kulamba waigizaji wa kike.....kwenye gari langu nimefunga mziki mnene na napiga mziki wa aina zote, na nyumbani pia
 
Lipa madeni mkuu,madeni hayapendi kelele.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mwana fa wakati anasoma na Mimi nilikua kwenye pilika za elimu,Ila nikaja kuona kazaliwa 1976,nikajipa moto,sema vyakula vya mgahawani sipendi,yaani nna masharti hatari,niliaguza chips dogo akaweka kachumbari wakati sikumwambia,aisee alienda kuikaanga Tena baada ya kutoa kachumbari,nikipita wananionesha vidole tu
 

Akili yako ilipevuka mapema.
Genius wengi ndio wapo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…