Sometimes hiyo ni njia ya kujipa moyo. Unakuta mtu ana dreams kubwa lakini hazifanyii kazi akitegemea maajabu.. Mfano mimi nilikuwa na ndugu yangu alipata pesa akafungua biashara kwa kutaka kuwakonga wabinti wenzake, duka kubwa frem kubwa ndani ina private ofisi, choo, kodi yake tu ni hatari. Nikamwambia hivi wewe unaanza biashara hii kodi mbona kubwa, jibu alilonipa sikurudia uliza. Kuendesha ile biashara cost ilikuwa kubwa sana kuliko mapato haikuchukua hata mwaka ikafa.
Maisha yake yakawa magumu, akaokoka, yeye ikawa ni kuomba tu Mungu amtendee miujiza. Hatafuti kazi waala hataki kuanzia chini na anadai karogwa. Yeye anaomba tu, ukimuona anakwambia flani ndiyo kaniroga kila mtu kuanzia ndugu, majirani, mwenye nyumba wake wote wachawi na ndiyo chanzo cha maisha magumu yake. sometimes failures zetu tunataka kuzibebesha watu. Maisha yake yalikuwa magumu hasa. Lakini mara zote ilikuwa anadai karogwa. aliuwa hafikirii huwezi kuwa kwa mwezi unaingiza kipato c halafu matumizi yako ni L ukategemea hutoanguka.
Ukifikria sana kuwa una maisha magumu kwasababu umerogwa, muda mwingi unakuwa unakosea. Una maisha magumu kwasababu huna connection, au hujajatafuta vya kutosha au umeridhika na maisha hayo magumu. Sikatai uchawi upo hata umetajwa kwenye vitabu vitakatifu ila watu wnautumia kama njia ya kujipa moyo kuwa wamefail kwasababu wamerogwa kama ambavyo vijana siku hizi tunajipa moyo kuwa kila kijana aliyefanikiwa anauza unga ila kujustify failures zetu.