Ukiona Mdada anakusalimia basi jiandae kwa haya yafuatayo

Ukiona Mdada anakusalimia basi jiandae kwa haya yafuatayo

Amekwama - anataka msaada wa pesa aka maokoto

Amepotea - anataka mtu wa kumwelekeza sehem anayoenda

Malizia....

Bandugu tusalimie sio hadi mkwame ndo mnarudi kutusalimia - tutawapotezea!
Kweli Kabsa
Kuna mdada nili mu approach zaidi ya miaka 2 iliyopita akazingua juzi Kati ananitafuta nikashangaa maongezi mengi mwisho kabsa n mkopeshe 200K
 
Jamaniiiiiiii😅😅😅
Fala wewe

Haupo romantic kama watu wafupi
Unataka nikubebishe hapa makima na manyani ya jf yanipopoe mawe?

Kuna mijitu hata ukicheka na demu humu inataka ikuwekee sumu ufie mbali😂😂😂
 
Unataka nikubebishe hapa makima na manyani ya jf yanipopoe mawe?

Kuna mijitu hata ukicheka na demu humu inataka ikuwekee sumu ufie mbali😂😂😂
Unaishi kwa kuogopa watu, tena wa jf? Acha hizo bana
 
Hamna kitu nachukiq kama kulisalimia li dada afu linaitika kwa kichwa as if ni bubu...Huwa nalichanaga hapo hapo sinaga salam za kuchezea
 
Hamna kitu nachukiq kama kulisalimia li dada afu linaitika kwa kichwa as if ni bubu...Huwa nalichanaga hapo hapo sinaga salam za kuchezea
Na ukilisalimia likaka likakujibu kwa kichwa unafanyeje?
 
ni kitu cha ajabu, kwamba mwanamke akikamatika kwenye shida kabisa, hata kama ni mke wa mtu, huwa yupo tayari kutoa mwili wake alimradi tu apate, iwe pesa, cheo au kazi. kuna mdada mfanyakazi, na tulimchangia pesa za arusi miezi minne iliyopita (though walikuwa wanabariki), leo kaja kwangu akapiga story akaondoka. baada ya dakika kama 10 ananiandikia msg anasema anaomba pesa akasukie. of course alipokuwa ofisini kwangu, nilikuwa najisikia vibaya kwasababu alikuwa anapoteza muda tu hana la maana alilokujia, na nikajua shetani anataka kuweka mtego kwangu.

kwanza nimejiuliza, nifanyeje, nikajua huyu ana shida ya pesa na amekamatika kwelikweli, pesa ya kusukia tu ninayo, ningeweza kumpa, lakini ana mume, mumewe akimuuliza umetoa wapi pesa ya kusukia atasema katoa wapi? na je, mimi ningekubali mwanaume mwingine ampe mke wangu pesa akasukie? Inawezekana mume wake hana hiyo pesa wiki hii na nywele zake anaona zinahitaji kusukwa ila je? nisemne hiyo ni necessary service kwenye maisha kwamba akikosa kusuka wakati anajipanga kutafuta maisha ataathirika? na ni mdada mzuri tu hata akinyoa atapendeza tu? nikafikia muafaka kwamba, sitampa pesa na nitampiga marufuku kuniomba pesa au kuwa karibu na mimi.

maishani, kabla sijamjua Mungu, nilikuwa dhaifu sana kwa wanawake. nilijifunza na kuhakikisha kwamba ni kweli, dawa ya uzinzi ni kufukia mashimo yote yanayoweza kupitisha uwezekano wa kuzini, hata ikibidi kimbia kwa miguu au kubali kugombana na mtu akuone humtaki alimradi tu usizini, kwasababu ukikaribia shina la uzinzi, utazini kweli na hakuna uzinzi ambao haujawahi kumsababishia mtu madhara, iwe kiroho au kimwili. hata ukiona kimwili upo safi tu jua kiroho kuna kitu kikubwa umepoteza. Mungu atusaidie sote.
Mungu atakushushia vingi kwa mtindo wa kukushangaza kama Zawadi ya ushindi[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Back
Top Bottom