Ukiona mtu ananunua papai ujue hana nyumba

Ukiona mtu ananunua papai ujue hana nyumba

Dhaumuni la mtoa hoja sio kazodoa watu wanaopanga ila kaonesha jinsi gani tunavyotakiwa kufanya tukiwa nyumbani Ili kuepuka manunuzi ya vitu rahisi ambavyo Tunaweza kufanya home.
Nakuelewa sana mkuu, ndio maana nimekujibu wewe zaidi nasio mtoa mada rejea comment yako ya juu.
 
Kama uko nyumbani kwako lazima upande mihogo,upande migomba,upande mipapai msitu wa matembere,lazima uweke vitu lazima upande vitu ule wewe na majirani waombe mboga za majani...Ukinunua papai wewe umepanga.
Wewe ndege hapa nyumbani nimepanda mapapai mpaka nimechoka. Hayaoti na hayataki kuota kwa sababu ya ardhi yenye mwamba. Nikaamua kuchimba shimo nika import udongo bado yakagoma. Mapapai na parachichi vyote vimegoma.

Kama hujui kaa kimya usimjudge mtu kwa kuangalia tu
 
Ni kweli ni raha sana , utatuaje mtu kapanga ila anazo nyumba kadhaa , na zina kila kitu , ila yupo kapanga sehemu fulani kwa sababu zake maalumu na papai ananunua tu?
Inatokea mtu amejenga mbali na shughuli zake za kujitafutia kipato Kwa hiyo anaamua kupangisha na yeye kukaa mjini karibu na kazini kwake
 
Kama uko nyumbani kwako lazima upande mihogo,upande migomba,upande mipapai msitu wa matembere,lazima uweke vitu lazima upande vitu ule wewe na majirani waombe mboga za majani...Ukinunua papai wewe umepanga.
Inategemea na eneo ulilonalo!
 
Vitu kama papai,embe,parachichi,passion in short matunda yote yenye mbegu haihitajiki kupanda wala kununua miche yake,yale yale unayonunua mbegu zake tenga sehemu kwenye ardhi yako zirushe.

Juzi jumapili nilikuwa nakagua home nina mapapai itabidi nipunguze miche,nina maembe miche sita (hii nitahamishia baadhi sehemu nyengine) nina miparachichi mitatu na passion nimeona moja,ipo miche sijajua kama ni ya limao au chungwa.
Safi kabisa!
 
Back
Top Bottom