Ukiona mtu ananunua papai ujue hana nyumba

Ukiona mtu ananunua papai ujue hana nyumba

Matatizo ya kukulia maporini mnadhani mijini viwanja ni bwerere tu. Hiyo square meter moja pekee ni kuanzia 15K sasa mpaka upate za kukutosha ijenge na ulime mapapai yako its not a joke. BTW kulima ni chaguo tu
 
Ni mtazamo wako tuu. Mwingine atakwambia kwake huo ni umaskini unakuta ameweka paving block nyumba nzima na bustani kidogo ya kitajiri kwaajili ya kufyeka majani.
Halafu anakwenda sokoni kununua chinese na spinach zilizopigwa dawa juzi yake.... Anakula na watoto...😅😂
 
kwamba gorofani na sio top floor kwenye veranda, unapandeje hivyo vitu ?

Hizi ndio generation ya mwisho mwisho watu wengi kumiliki uwanja wa kujinafasi sasa hivi wameanza kutoa hati ya apartment yako tu na ardhi mnashare watu lukuki
 
Mtu akinunua pembezoni na mji anaweza kupata viwanja vikubwa akafanya kama hayo,lakini viwanja vilivyo vingi unajenga nyumba inabaki sehemu kidogo mbele kiwanja kimeisha.
Mkuu nimegundua hivi vitu ni hobie ya mtu asee. Mimi kuna jirani yangu hadi huwa namuonea huruma.
anakiwanja kikubwa kifupi tu ni shamba ni zaidi ya heka ila hulima mahindi lote ajabu ni kwamba hana tunda hata moja! mimi nimehamia nyuma yake lakini papai anatoa kwangu pilipili anatoa kwangu mapassion na limao

Mwezi wa3 nikakuta mapassion mengi sana yamejiotoea jalalani nikayahurumia na kuyabeba nikampa nayeye nikimsadia na kuchimba shimo moja la mfano baada ya kutoka tu hapo kwake kazi akaachia watoto!! na watoto hakuna walichofanya!!

Shimo lipo empty hadi dk hii. Kwake kuna mbomba la maji ila hakuna hata tembelee moja la dawa kwa kifupi jamaa hawazi na anapenda matunda hata tukiwa kitaa anaweza kukuomba umtoe 5000 anunue matunda na anakurudishia hela yako ila kupanda sasa hana habari.

Jamaa hata kuku hana hapo kwakwe ila ana mbwa 6 na anawalisha vizuri tu anakwambia mbwa ndo kila kitu ...kwa kifupi huyu jamaa ni basi tu.,

Nije kwenye point yako ya kiwanja siyo kweli mkuu papai hata likipandwa karibu na msingi wa nyumba yako halina jamu kabisa na hii nimeona mimi kwa dada yangu. huwa likikua kabisa analikata muda huo kuna mpapai mwingine umeanza kuiva.

Mimi kila nilipokuwa na panga iwe single room nikimaliza miezi3 lazima nilete kuku hata wawili nilikuwa nalala nao wao kwenye box wala hamna shida hata wasipozaa sio issue zangu kuwaona vile raha mno najisi nimekamilika kabisa.
 
Back
Top Bottom