Ukiona Mwembe umejaa Maembe yaliyoiva kwenye Nyumba yenye Watoto watukutu basi kuna mawili

Ukiona Mwembe umejaa Maembe yaliyoiva kwenye Nyumba yenye Watoto watukutu basi kuna mawili

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Ukiona Mwembe umejaa Maembe yaliyoiva na kuning'inia kiasi cha kuvutia kwenye nyumba ya watoto watukutuku au shule basi tambua kuna haya mawili;

1. Huenda Mzee mwenye mwembe ni mkali sana au Mchawi
2. Maembe ni machungu balaa yasiyolika hata kwa chumvi!

Kwa mfano ule ule utumie pia unapoona Mrembo/Mkaka wa makamo Ambaye hajaolewa/oa Usikurupuke kuingia kichwa kichwa lipo jambo!

Vuta subira!

Tambua kwamba kama kwa jirani Maembe kama hayo yanaliwa na chumvi yakiwa machanga! Iweje Hayo yakomae yakiwa mtini?

"Ukiwa naye ndipo utaelewa kwanini ulimkuta Single "
 
Mkuu kwa fact hii, petition ya kujengewa sanamu lako pale Posta inaanzishwa muda si mrefu
Watu wengi sana wameangamia kwa kuingia kichwa kichwa! Wewe unaona kabisa watu wamesimama nyomi pembeni kuna kiti kiko wazi!

Wewe unafika pasipo kutafakali unabandika makalio.....hakika kuna mawili! Either kiti kibovu au ni cha kiongozi/dereva! Jiandae kunyanyuliwa
 
Kwenye maembe sawa, lakini kwenye mahusiano umebugi step,

Siyo lazima mtu kuoa/kuolewa kwa sababu haya ni maamuzi binafsi.

Hakuna aliewai kuripotiwa kupata tatizo la akili kwa sababu hakuwa ameoa/ kuolewa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Kitendo cha kutoolewa au kuoa hadi makamo yasogee lazima kuwepo sababu!

Rai yangu ni lazima kuwepo tafakari ya kina watu wanaoingia kwenye hayo mahusiano!
 
Maembe ni maembe na mtu wa makamo ni wa makamo, Tusitishane😂😂😂, ndiyo namtumia sms hapa huyu binti wa makamo😂😂
Tunatishana Sana, Vigogo Wapukutika, Vigogo Wafa Ni Uzushi Mtupu, Tuchape Kazi Ndugu Zangu!! Bwana Bure Hayupo
By Jiwe
 
Huwezi kufananisha maembe na binadamu kwasababu binadamu anamipango yake na maamuzi yake ya kuamua mambo,mwingine haoi wala kuolewa bila kuaccomplish mambo fulani.
Hiyo ni justification ya kukinga udhaifu!

Ndiyo maana tunakumbushwa kutafakali! Mfano!

Anaweza akawa anajipanga lakini huko mtaani akazalisha wanawake kibao! Then anakuja kuoa nyuma analea mitoto kibao!
Au anaweza akawa mwanadada anajipanga lakini katoa mimba kama 800!

Au anaweza kuwa anajipanga kumbe anangoma!

Au anaweza kuwa anajipanga kumbe ni mwezi mchanga (waruwaru) lakini huwezi kujua hadi awe mpenzi wako!

NDIYO MAANA NIKASEMA UKIONA KINANG'AA single KIICHUNGUZE KWANZA LAZIMA KUNA JAMBO!
 
Maembe yanaliwa machanga sembuse machungu. Kuoa/kuolewa ni maamuzi ya mtu. Kulala na kuamka kitanda kimoja na mtu huyo huyo for the rest of you life sio kila mtu anaona ni sahihi kwake.
 
Back
Top Bottom