Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Huenda Mzee mwenye muembe ni mkali sana au Mchawi[emoji23]Ukiona muembe umejaa maembe yaliyoiva na kuning'inia kiasi cha kuvutia kwenye nyumba ya watoto watukutuku au shule basi tambua kuna haya mawili;
1. Huenda Mzee mwenye muembe ni mkali sana au Mchawi
2. Maembe ni machungu balaa yasiyolika hata kwa chumvi!
Kwa mfano ule ule utumie pia unapoona Mrembo/Mkaka wa makamo Ambaye hajaolewa/oa Usikurupuke kuingia kichwa kichwa lipo jambo!
Vuta subira!
Tambua kwamba kama kwa jirani maembe kama hayo yanaliwa na chumvi yakiwa machanga! Iweje Hayo yakomae yakiwa mtini?