Ukiona ndugu na watu wanamdharau Mkeo ujue wewe mwenyewe Wanakudharau

Ukiona ndugu na watu wanamdharau Mkeo ujue wewe mwenyewe Wanakudharau

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UKIONA NDUGU NA WATU WANAMDHARAU MKEO UJUE WEWE MWENYEWE WANAKUDHARAU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Huwezi kuwa Mwanaume mwenye heshima kama Mkeo anadharaulika, na kudharauliwa na watu wengine. Iwe ni wazazi au ndugu zako ukiona Wanamdharau Mkeo ujue hata wewe wamekudharau, wanakuchukulia oyaoya! Kwa kifupi wewe huna lolote.

Chain inaendelea, ukiona Mkeo Wanamdharau ujue hata watoto wako wanadharaulika, wanadharauliwa.

Haiishii hapo, sasa Mkeo anadharauliwa na watu, watoto nao vivyohivyo, kinachofuata ni watoto na Mkeo kukudharau.

Mtoto hawezi kumheshimu Baba yake ikiwa Mama yake anadharauliwa na watu wengine wakati Baba yupo. Never ever!

Heshima ya Mwanaume kama Baba inajengwa na Mambo Makuu yafuatayo;
1. Upendo wa Baba kwa Familia yake.
Ili Baba aheshimike katika familia yake lazima, narudia ni lazima aipende familia yake kuliko kitu chochote kile.
Baba anayeipenda familia yake kuliko kitu chochote kile huheshimiwa na mke na watoto wake kuliko yeyote Yule.
Hii ni kusema, upendo wa Baba ni proportional na heshima atakayopewa.

Kadiri unavyoipenda familia yako ndivyo watu wengine watakavyoiheshimu familia yako yaani Mkeo na watoto.

2. HAKI.
Ili mwanaume kama Baba ajenge Legacy katika familia na ukoo atakaouanzisha, watoto na Mkewe wampende lazima ajue kutenda HAKI kwa familia yake.
Sheria, kanuni na taratibu ambazo Baba au mwanaume utaziunda ndani ya familia yako lazima zizingatie HAKI.
Haki za kiumri
Haki za kijinsia.
Haki za kimaumbile.
Haki za kiwakati.
Haki za kijumla yaani za watu wote.
Mamlaka, majukumu na wajibu ya members wa familia lazima yazingatia HAKI na yawe na mantiki.

Kama Baba lazima Ujitahidi kuwa role model katika kufuata Sheria, kanani, na taratibu mlizojiwekea ndani ya familia ili kuonyesha kuwa Sheria hizo zinatekelezeka, na wote mpo sawa ndani ya familia lakini hamlingani.

Ukiweza kutenda HAKI kwa Mkeo na watoto wako, automatically ndugu na watu wengine hawawezi kumdharau Mkeo na watoto.

3. MAENDELEO KUPITIA KUFANYA KAZI.
Kama Baba na mwanaume lazima uhakikishe Mkeo na watoto wanatija ndani ya hiyo familia.
Kupitia vipawa, karama, ujuzi na elimu wa kila Mmoja wa Memba wa familia lazima azalishe au aingize chochote ndani ya familia.

Mkeo kama sio mzalishaji ni rahisi ndugu zako na watu wengine kumdharau kwa sababu mtu yeyote asiyezalisha ni kama maiti tuu.

Kuzaa hata panya wanazaa. Kulea hata mbwa wanalea.

Iwepo mipango ya kifamilia, iundwe miradi ya kifamilia na kila Mmoja apewe mradi wa kusimamia kulingana n uwezo, ujuzi, umahiri na elimu ya Memba katika mradi husika.
Ziwepo Sheria za mapato na matumizi kwa kila memba mzalishaji katika mradi husika.
Mfano,
Kila memba kupitia mradi atakaopewa ausimamie atalazimika kuonyesha mauzo na faida kwa kila mwezi. Asilimia 75% ya faida itakayozalishwa itawekwa kwenye akaunti ya familia ya pamoja.
Asilimia 25% ya faida itakuwa kifuta jasho kwa Memba husika katika mradi huo aliousimamia na ataitumia katika mambo yake binafsi lakini ya Halali.
Yaani kama kwa mwezi faida ni laki Moja, basi Tsh 75,000/= itawekwa kwenye akaunti ya familia huku Tsh 25,000/= akichukua memba msimamizi wa mradi kwa matumizi yake binafsi.

Hata hivyo matumizi ya kila memba wa familia kwa mwezi lazima yawe yameshajulikana na bajeti yake ilishatolewa na kukabidhiwa kila memba kulingana na atakavyopendekeza. Kama mtu atapendekeza apewe Cash atapewa Cash. Na kama atataka awekewe kwenye akaunti yake binafsi vivyohivyo.

25% ya Faida haitahesabika katika sehemu ya pesa atakayopewa mtu husika.

Kwenye faida itatolewa tena 10% kwaajili ya Fungu la Kumi kwaajili ya Zaka kwa Mungu.
Hii itawekwa kwenye akaunti ya Zaka ya familia yenu kwa kila Mmoja wenu.

10% itatolewa kwa Watumishi wa Mungu mnaowaamini Sana kuwa wanatenda Kazi za Mungu. Kama hakuna watumishi hao yaani ikiwa familia itaona kuwa Watumishi hao hakuna na wengi wamekaa kibiashara basi pesa hiyo mtaipeleka kwa wahitaji kama wajane, yatima, chokoraa au wafungwa.

Mtaikusanya kwa mwaka mzima kisha mtanunua kama ni nguo sharti ziwe mpya, au sabuni, au chakula sharti kiwe kizuri na standard na cha heshima, au kitu chochote ambacho ni hitaji la msingi kwa wahitaji.

Lazima mapato yawe wazi.
Ingawaje lazima iwepo Sheria ya baadhi ya mapato yawe siri ya Baba pekee kwa ulinzi na usalama wa Familia.

Nilisema lazima HAKI itendeke kulingana na umri, jinsia, maumbile, nyakati n.k.
Ndio maana kuna baadhi ya maeneo Baba/Mume anaweza Kupata HAKI zaidi kuliko Mama/mke.
Halikadhalika yapo mazingira mke/Mama hupata HAKI zaidi kuliko Mume/Baba.

Hata yapo mazingira ambayo Watoto hupata HAKI zaidi au tuite upendeleo zaidi kuliko wazazi(Baba na Mama).
Mfano, chakula ni kidogo ndani ya nyumba, watoto inatarajiwa wapewe upendeleo zaidi kuliko wazazi.

HAKI inaenda sambamba na upendo. Lakini vyote viwili haviwezi kuwa na Tija kama hakuna AKILI na MAARIFA.

Tukirudi kwenye Mada.

Usimnenee Maneno Mabaya Mkeo mbele za watu ili kulinda heshima yako. Unapomnenea Mabaya Mkeo mbele za watu wakiwemo ndugu zako unamdharaulisha na hiyo itawapa watu kibali cha kumdharau na kukudharau wewe.

Hata Baba yako mzazi au Mama yako mzazi Hana ruhusa ya kumnenea Mabaya Mkeo. Kumtukana au kumkejeli ni dharau kwa familia yako na wewe MWENYEWE.

Ukishaanzisha familia yako lazima uelewe wewe ni serikali inayojitegemea na kujitawala. Hakuna mwenye mamlaka yoyote ya kuingilia nyumba yako.

Ni laana, ni anguko kuu kuruhusu serikali zingine ikiwemo ya wazazi wako kuingilia nyumba au serikali yako.

Kuna sheria ya mipaka, usisogeze Mpaka wa jirani yako Wala jirani yako asisogeze Mpaka wako. Kiroho unapata Laana kusogeza Mpaka wa jirani yako au kuruhusu Mpaka wako usogezwe.

Kusogeza Mpaka ni sehemu ya tafsiri ya kudharauliwa.

Yaani mtu kukuingilia kwa mambo yasiyomhusu. Kukufanyia maamuzi, kumtusi Mkeo au watoto wako. Huko ni kusogeza Mpaka wako. Kamwe usikubali.

Kuna mipaka ya aina nyingi.
Mipaka ya kifamilia, yaani kila familia inamipaka yake. Usikubali familia nyingine hata ya wazazi wako kuingilia familia yako au wewe kuingilia familia ya wazazi wako hiyo ni dharau na Laana.

Kuna mipaka ya mtu Binafsi.
Yaani wewe umemuoa mke wako lakini kuna mambo hupaswi kumuingilia hasa maamuzi yake binafsi. Mfano kama mwanamke amekengeuka, au anataka kukuacha usimlazimishe abaki kwenye maisha yako.
Unaweza mshauri lakini ushauri usizidi mara tatu.
Hivyo ndivyo watibeli tunavyofanya mambo yetu.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Una tafsiri yako ya heshima mkuu?
We heshima ya mtu kwako utaitambuaje?
Kuna heshima, unafiki na utii
Kaa utafakari haya

Heshima ni Hisia au kitendo chanya ambacho Watu huonyesha kama sehemu ya kuthamini, kujali na kukubali mtu au Jambo zuri

Heshima ni matokeo ya HAKI
Heshima yoyote isiyotokana na HAKI huitwa UNAFIKI.

Utii ni kukubali maelekezo, kusikiliza maelekezo na kuyafanya
 
Nafikiri hujui vitu vingi sana kuhusu ndoa mdogo angu, kaa kimya huku ukijifunza taratibu

Nijifunze kwako au kwa Nani?

Watu waliokaa kimya wote wamejifunza?

Ungetoa hoja hata Moja ingesaidia wasomaji wengine lakini sio ajabu wewe ni wale watu ambao hawana wanachojua na hawana uwezo wa kuwajulisha wengine na bado utawaambia watu wakae kimya.

Hoja yako hasa ni nini?
 
Heshima ni Hisia au kitendo chanya ambacho Watu huonyesha kama sehemu ya kuthamini, kujali na kukubali mtu au Jambo zuri

Heshima ni matokeo ya HAKI
Heshima yoyote isiyotokana na HAKI huitwa UNAFIKI.

Utii ni kukubali maelekezo, kusikiliza maelekezo na kuyafanya
Kama heshima ni hisia
Utamtambuaje hisia za mtu dhahiri
Ni ngumu kugundua furaha ya kweli ya mtu
Unaweza kudhani unaheshimika kumbe kinyume chake
We Fanya unachoweza ila usingoje heshima
Heshima sio malipo au kipigo ya chochote
 
Kama heshima ni hisia
Mbona umeikatisha maana niliyoandika.
Utamtambuaje hisia za mtu dhahiri
Ni ngumu kugundua furaha ya kweli ya mtu
Sio ngumu kutambua au kugundua furaha ya kweli ya Mtu.
Jambo lolote zuri linampa mtu furaha.
Watu wote wanapenda na kufurahia kuheshimiwa na kupendwa.
Ukimfanyia mtu Jambo lolote zuri lazima afurahie. Wala sio hiyari.

Ukimfanyia mtu Jambo Baya lazima achukie na kuhuzunika Wala sio hiyari.

Huo ugumu wa kutambua na kugundua hisia za watu unatoka wapi?


Unaweza kudhani unaheshimika kumbe kinyume chake.

Ukifanya Jambo lolote zuri na jema matokeo yake ni heshima.

Hata hivyo lazima ujue kila Jambo Lina expired date. Sio ufanye Jambo jema miaka ya tisini huko utegemee hilohilo ndilo ulitumie kuheshimika Mpaka hivi Leo
We Fanya unachoweza ila usingoje heshima.
Heshima ni basic needs kwenye nafsi ya mtu.


Heshima sio malipo au kipigo ya chochote

Heshima ni malipo au matokeo ya matendo, Maneno yako.

Watu hawawezi kukuheshimu from nowhere
 
Ili mtu ajue mambo ya ndoa anatakiwa awe ameoa for how long?

Unataka upige ramli sio?
Just an answer mdogo angu, huna haja ya kupiga siasa!!. Umekaa kwenye ndoa kwa miaka mingapi??
Usije ukawa unafundisha watu ndoa kumbe hujaoa au umeacha/achwa(ndoa imekushinda) au ndio kwanzaaaa una miaka miwili.

How long bwana mdogo?? Maana si kila mtu ana qualify kufundisha haya mambo
 
Just an answer mdogo angu, huna haja ya kupiga siasa!!. Umekaa kwenye ndoa kwa miaka mingapi??
Usije ukawa unafundisha watu ndoa kumbe hujaoa au umeacha/achwa au ndio kwanzaaaa una miaka miwili.

How long bwana mdogo?? Maana si kila mtu ana qualify kufundisha haya mambo

Unachokifanya ni kutaka kupiga ramli.

Kwako ndoa ni kitu gani?

Sio ajabu nipo kwenye ndoa miaka mingi kuliko wewe
 
Back
Top Bottom