Ukiona ukatili mtandaoni, usikae kimya na Usishiriki. Tunaweza kubadilisha mtandao uwe salama kwa kila mtu

Ukiona ukatili mtandaoni, usikae kimya na Usishiriki. Tunaweza kubadilisha mtandao uwe salama kwa kila mtu

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Je, umewahi kuona chats za watu zikisambazwa mitandaoni huku wengine wakicheka na kuendelea kuzishare? Wengine huenda mbali zaidi kwa kutaja majina ya wahusika, vyeo au hata ndugu zao nk.

Huo ni ukatili wa mtandao kwani mawasiliano mengi hufanyika kwa faragha kati ya watu wanaoaminiana. Pale ambapo mmoja anavunja uaminifu na kusambaza mazungumzo hayo hadharani, anakuwa amefanya ukatili kwa kumuabisha na kumuumiza mwenzake.

Kusambaza chats za siri ni kuvunja faragha, ni aina ya unyanyasaji wa mtandaoni na inaweza kusababisha madhara makubwa ya kihisia na kijamii

Wakati mwingine, hata kwenye mahusiano, ni muhimu kujilinda, hebu usijimalize kupita kiasi bila tahadhari kwani si kila anayesema anakupenda ana staha ya kulinda heshima yako, wapo wanaoweza kutumia mawasiliano yenu kukuumiza baadaye.

Ukiona ukatili mtandaoni, usikae kimya bali kemea au ripoti ili hatua zichuliwe na usishiriki kusambaza au kuchochea ukatili huo kwani kwa kufanya hivyo tunaweza kubadilisha mtandao uwe salama kwa kila mtu.
  • Tusishiriki maudhui ya kuaibisha wengine
  • Tusichekelee ukatili wa kijinsia mtandaoni
  • Tulinde faragha za watu
  • Tuseme hapana kwa OGBV
Ukatili wa kijinsia mtandaoni sio sawa. Chukua hatua. Linda wengine. Linda utu

Pia soma:

 
Back
Top Bottom