The world wishes well for no damn body. Ukiwa na chako kizuri, stay low, enjoy peke yenu. Labda occassionally ndo uyaweke public. Lakini kila mara kujitahidi kuonyesha mapenzi yako/yenu katika kadamnasi, I believe katika mtu 10:mtu 1 ndo atawafurahia, wengne tisa tutamani kila aina ya baya liwatokee. It is what it is.
Naamini low profile katika ndoa, mapenzi , mahusiano ni nzuri, ili yoyote yatakayotokea m-baki kuyatatua wahusika na sio jamii. Jamii huwa inaappreciate ugomvi, utengano, mabaya. Ndo maana topic za mambo ya michepuko, kimasihara, usaliti, zina comments nyingi kuliko topic za kujenga katika nyanja ya ndoa ama mahusiano.
Kila kukicha ni malalamiko, mwanamke huyu, mwanaume huyu kanifanyia this or that. Maybe unionyeshe topic yenye wachangiaji wengi ambayo imelenga kurestore broken homes ama kuwaasa vijana na wazee ili kudumu katika familia, nitakuonyesha twiga ANAYEPAA.