Ukiona wenzako wanavyofanya ufugaji wa kuku, Mabanda yao walivyojenga, kwa hakika hutaacha kufuga

Ukiona wenzako wanavyofanya ufugaji wa kuku, Mabanda yao walivyojenga, kwa hakika hutaacha kufuga

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
961
Reaction score
533
Ufugaji wa kuku Tanzania kwa sasa umeshika kasi, watu wameelimishwa wakaufahamu ufugaji huo. Ufugaji wa kuku unaofanywa ni wa aina mbalimbali kuna wanaofuga kuku wa nyama broilers, kuku wa mayai wa kisasa layers, machotara crossbreeds na hata wale wanaofuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya mayai na nyama. Kuna wengine pia wanajihusisha na miradi ya utotoreshaji wa vifaranga wakati wengine wakiwa wanafuga kware, Bata mzinga, Kanga nk ili mradi tu kila mtu anafuga kile anachotaka.

Katika mjadala huu nimeona niwatembeze katika miradi mbalimbali ya wafugaji, tuone ufugaji wao mabanda yao, mifugo yao nk ili kupitia kuona huko, naamini kuna kitu tunaweza kujifunza lakini pia kupata hamasa ya kufuga na hivyo kujikwamua kiichumi na kuweza kuondokana na dhana ya kutegemea kuajiriwa.


Lakini pia kupitia mada hii kama utahitaji kuku wa aina yoyote au mazao yake kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii, mahoteli, migahawa nk utapata kwa bei nafuu kabisa. Vilevile tunauza vifaranga wa kware na mayai yake kwa idadi yoyote utakayoihitaji. Kwa mahitaji yako basi usisite kuwasiliana nami na kama ukihitaji namba yangu nitakupm tafadhali. Kwanini tulalamike hakuna kazi wakati kuna fursa za kutosha nchini. Tafakari chukua hatua, umasikini haukubaliki.

Picha chini ni kuku wa nyama aina ya Kenbro wakiwa tayari kwenda sokoni.

IMG_20140914_110355.jpg IMG_20140914_110359.jpg IMG_20140914_110351.jpg kuku 3.jpg kuku 4.jpg
 

Attachments

  • Vifaranga wa kienyeji wakiwa katika Bruda.jpg
    Vifaranga wa kienyeji wakiwa katika Bruda.jpg
    77.7 KB · Views: 2,475
Hawa ni kuku wa mayai wenye umri wa wiki 15 jumla yao wakiwa 1000. Ukiwatazama utagundua kuwa ni kuku wenye afya njema waliofugwa kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji wa kuku. Wamekaa kwa nafasi vyombo vya kutosha vya maji na chakula. Ni kuku wanaofugwa na dada Honoratha Nchimbi wa Nkuhungu Dodoma kwa ushauri wangu. Yeye alianza kukupata shauku ya kufuga baada ya kufuatilia mada yangu https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/Ni kwa wafugaji/wanaotaka kuanzisha mradi wa ufugaji kuku.Alifanya jitihada ya kunitafuta na mwishowe alinipata na kumshauri, leo kapiga hatua. Kuku hawa watakapofikia umri wa wiki 19 wataanza kudondosha mayai.

kuku mayai 1.jpg kuku mayai 2.jpg kuku mayai 2.jpg Kuku mayai 4.jpg Kuku mayai 5.jpg
 
Wamependeza sana...
Nimejaribu kuku ishirini, ila wamevamiawa na ndui....wataalamu wanasema hakuna tiba. Ila natumai watapona maana niliambiwa niwape otc plus...nimeanza kuwapa.
 
Hawa ni vifaranga wa kuku wa kienyeji wakiwa katika bruda na wengine wakiwa katika hatua ya ukuaji nje ya Bruda. Hatua ngumu zaidi ya utunzaji vifaranga ni hii ya kwenye bruda kweni kipindi hiki vifaranga wanahitaji uangalizi wa hali ya juu ili waweze kukua vyema. Joto sahihi linahitajika wakati wote katika kipindi chote cha wiki tatu lakini sana sana zile wiki mbili za mwanzo.

Mwanga nao katika kipindi hiki ni muhimu ili waweze kupata nafasi ya kula chakula chao cha vifaranga , chicks starter mash kitakacho wawezesha kukua vizuri.

Katika kipindi hiki ni muhimu pia mfugaji akazingatia kwamba ni kipindi ambacho vifaranga wakati mwingine huwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa kitovu kutokauka vizuri kitu ambacho huweza kusababisha kuvamiwa na bacteria na kuozesha hivyo kusabisha vifo kwa vifaranga. Ugonjwa wa matumbo aina ya Pullorum/ white bacillary diarrhea, ugonjwa wa kuhara damu coccidiosis vilevile yanapaswa yatazamwe kwa umakini kwa kuwa ni kati ya magonjwa yanayosababisha vifo vingi kwa vifaranga.

Ni muhimu hatahivyo, kwa vifaranga watakapofikia umri wa wiki moja wakachanjwa chanjo dhidi ya ugonjwa mdondo/kideri na watakapofikia siku ya kumi na nne wachanjwe chanjo dhidi ya ugonjwa wa Gumboro. Siku ya 21 warudiwe chanjo wa mdondo.

Vifaranga wakilelewa vizuri huwa hawasumbui hata kidogo.

View attachment 217788 View attachment 217789 View attachment 217789 View attachment 217790
 
Hapa vifaranga wa mayai ndiyo kwanza wametoka kuzaliwa. Baada ya kuzaliwa kazi inayofuata ni kazi ya kuchambua na kubaini yupi tetea na yupi ni jogoo (sexing) kazi ambayo hufanywa kwa utaalamu wa hali ya juu maana ni rahisi sana kukosea hasa kama kuku wazazi ( parent stock) baba na mama wote wanapokuwa na rangi moja maana yake hata wale vifaranga watakaozaliwa nao watakuwa na rangi moja wote watakuwa weusi kwa kufuata rangi za wazazi wao. Uchambuzi huu hufanywa kwa kutazama mabawa yao mara tu baada ya kuzaliwa.

Vifaranga hao chini wamezalishwa na hatchery inayoendeshwa na Matembwe Village Co. Ltd, hatchery hii iko Matembwe, Lupembe kilometa 60 kutoka Njombe mjini.

Ili utotoleshe Vifaranga unahitaji uwe na mashine(Incubators) pamoja na kuku wazazi walio na uwiano Jogoo mmoja kwa Tetea 10 ili kupata mayai yaliyorutubishwa vyema. Aina ya parent stock itategemea na aina ya mahitaji yako, kwamba ni aina gani ya kuku unataka kuwaalisha na kuwauzia wateja wako.

View attachment 217792 View attachment 217793 View attachment 217794 View attachment 217795
 
Kuku wa mayai wanachukua gharama nyingi kuwalisha daaa unawahangaikia kinoma ila ikishafika mida ya kuvuna mayai ni raha iliyoje aisee yan unavuna trei kadhaa huku unamwinua mungu
 
Kuku wa mayai wanachukua gharama nyingi kuwalisha daaa unawahangaikia kinoma ila ikishafika mida ya kuvuna mayai ni raha iliyoje aisee yan unavuna trei kadhaa huku unamwinua mungu

Ungefunguka changamoto zake na zaidi mafanikio uliyoyapata manake yanaweza kuniinspire zaidi kwani nina mpango mwezi huu nikamilishe huu mradi.
 
Hongera sanaa mkuu,thread nzuri sanaa,kwa wale wote walioko Dar na mikoa ya karibu,mnaweza pata kuku wa nyama na wayai,pamoja na vijogoo kwa bei nafuu kabisa na raisi kufuga.

Broiler (Nyama) ni TZS 1300
Layers (Mayai) no TZS 2200
Vijogoo (Male Layers ) ni TZS 40
Hizi ni bay per DOC na ndani ya box wanakaa 102.

Vifaranga toka breed bora kabisa ya ISA BROWN NA ARBOR ACER.

NITAFUTE KWENYE NO 0717332652,Kwa wale ambao mmeshanunua kwangu mnaweza elezea ubora wa bizaaa zangu.

KUKU WANALIPA SANA,JIAJIRI MAISHA YATAENDA TU.
 
Uchambuzi huu hufanywa kwa kutazama mabawa yao mara tu baada ya kuzaliwa.

Naomba ufunguke zaidi ili tuweze kuelimika vizuri katika kutenganisha mitetea na majogoo wakiwa wana siku 1 - 7
 
Nimeipenda sana hii...thanks to JF kwa kutuletea habari tofauti zitakazo tufanya kusonga mbele...
 
Hongera sanaa mkuu,thread nzuri sanaa,kwa wale wote walioko Dar na mikoa ya karibu,mnaweza pata kuku wa nyama na wayai,pamoja na vijogoo kwa bei nafuu kabisa na raisi kufuga.

Broiler (Nyama) ni TZS 1300
Layers (Mayai) no TZS 2200
Vijogoo (Male Layers ) ni TZS 40
Hizi ni bay per DOC na ndani ya box wanakaa 102.

Vifaranga toka breed bora kabisa ya ISA BROWN NA ARBOR ACER.

NITAFUTE KWENYE NO 0717332652,Kwa wale ambao mmeshanunua kwangu mnaweza elezea ubora wa bizaaa zangu.

KUKU WANALIPA SANA,JIAJIRI MAISHA YATAENDA TU.

Samahani mkuu, hapo pekundu hapajakaa sawa, hiyo 40 ni US $ au Tzs, fafanua kidogo.
 
Samahani mkuu, hapo pekundu hapajakaa sawa, hiyo 40 ni US $ au Tzs, fafanua kidogo.
Pako sawa kabisa mkuu,namaanisha kwa lugha nyingine,TZS 40,000 Kwa box moja lenye vifaranga 100.

Kama uko tayari number yangu ni 0717332652.
 
Back
Top Bottom