Mkuu nakuaminia broiler wako wazuri sana. Hawa vijogoo wanapanda I mean wanafaa kwa mbegu au ndo kula tu? Max uzito wao kiasi gani? Na umri gani wanauzwa?
Wanakuwa na rangi nyeupe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanakuwa na rangi nyeupe.
Mkuu nakuaminia broiler wako wazuri sana. Hawa vijogoo wanapanda I mean wanafaa kwa mbegu au ndo kula tu? Max uzito wao kiasi gani? Na umri gani wanauzwa?
Jogoo yeyote anapanda,hawa pia wanapanda kama kawaida,kuuzwa as kama utawafuga kienyeji ni kuanzia 13 weeks,but wanakuwa majogoo makubwa sanaaaaaaaa
Thanks nimekupata mkuu nitakutafuta mie napenda vitu unique ili kuwa na brand tofauti. Nitakujulisha lini nikiwa tayari
Ufugaji wa kuku Tanzania kwa sasa umeshika kasi, watu wameelimishwa wakaufahamu ufugaji huo. Ufugaji wa kuku unaofanywa ni wa aina mbalimbali kuna wanaofuga kuku wa nyama broilers, kuku wa mayai wa kisasa layers, machotara crossbreeds na hata wale wanaofuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya mayai na nyama. Kuna wengine pia wanajihusisha na miradi ya utotoreshaji wa vifaranga wakati wengine wakiwa wanafuga kware, Bata mzinga, Kanga nk ili mradi tu kila mtu anafuga kile anachotaka.
Katika mjadala huu nimeona niwatembeze katika miradi mbalimbali ya wafugaji, tuone ufugaji wao mabanda yao, mifugo yao nk ili kupitia kuona huko, naamini kuna kitu tunaweza kujifunza lakini pia kupata hamasa ya kufuga na hivyo kujikwamua kiichumi na kuweza kuondokana na dhana ya kutegemea kuajiriwa.
Lakini pia kupitia mada hii kama utahitaji kuku wa aina yoyote au mazao yake kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii, mahoteli, migahawa nk utapata kwa bei nafuu kabisa. Vilevile tunauza vifaranga wa kware na mayai yake kwa idadi yoyote utakayoihitaji. Kwa mahitaji yako basi usisite kuwasiliana nami na kama ukihitaji namba yangu nitakupm tafadhali. Kwanini tulalamike hakuna kazi wakati kuna fursa za kutosha nchini. Tafakari chukua hatua, umasikini haukubaliki.
Picha chini ni kuku wa nyama aina ya Kenbro wakiwa tayari kwenda sokoni.
View attachment 217763 View attachment 217766 View attachment 217767 View attachment 217769 View attachment 217770
Jembe langu mama Joe aminia sana,kwanza napenda tunavyofanya business though hatujawahi onana,hope soon wale broiler utauza,kama wakifikisha kilo 1.4,nitakuja kuwanunua if possible.

Inapendeza. Mi ningependa kujua kutoka kwa wazoefu, soko la kuku na mayai linapatikana vipi kwa mtu atayejitosa ktk ufugaji kuku? Natanguliza shukrani.
Inapendeza. Mi ningependa kujua kutoka kwa wazoefu, soko la kuku na mayai linapatikana vipi kwa mtu atayejitosa ktk ufugaji kuku? Natanguliza shukrani.
Kwa uzoefu wangu ni kwamba Soko la kuku Tanzania ni kubwa lakini changamoto iliyopo ni kuwa chakula cha kuku ni ghali sana ukilinginisha na bei ya mayai. Ushauri wangu kwa wafugaji wa kuku hasa wa mayai kuhakikisha kuwa chakula utakachotengeneza kitengenezwa kwa gharama nafuu ili kupunguza gharama na kujiongezea faida.
Namna ya kupunguza gharama ni pamoja na kununua mahitaji ya kutengenezea chakula cha kuku wakati wa msimu wa mavuno ambapo bei zake huwa ni ndogo.