Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ufugaji wa Kware kwa sasa umekuwa wenye tija kubwa hasa kutokana na kware mwenyewe pamoja na mayai yake kutumika kama dawa kwa watoto na wazee. Kutokana na matumizi hayo, mahitaji ya kware na mayai yake yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku. Kwakuwa mahitaji ni makubwa kuliko uzalishaji wake, umefanya bei ya mayai na kware kuwa kubwa. Kwa sasa Bei ya kware inakwenda hadi tsh 30000/= wakati bei ya yai moja ni shilingi 1000/= kwa hiyo ukiwa na tray moja utaliuza kwa shilingi elfu thelathini.
Utunzaji wa Kware kimsingi hawana tofauti na utunzaji wa kuku. Hata kwenye upande wa chakula, ambacho kware anakula ni kama kile ambacho kuku anakula. Kitu muhimu cha kuzingatia ni kwamba kifaranga wa kware haitaji maji hata kidogo. Kifaranga wa kware akiloa maji unampoteza mara moja.
View attachment 219415 View attachment 219417 View attachment 219418 View attachment 219419 View attachment 219420 View attachment 219421
Bei ya kifaranga mmoja wa kware wa siku moja ni tsh 2700, wa wiki moja ni tsh 3800, wa wiki 2 ni tsh 10000/= Mayai ya kware tray moja kwa bei jumla tunauza elfu 18,000/=
Second Lieutenant unaweza ukaweka picha ya hao majogoo wakiwa na wiki ya 13 tayari kwa kuuzwa? Nimevutiwa nao...
Wanakuwa na kg ngapi ukiwafuga kwa mfumo wa Layers?
Aman Ng'oma.........hizi picha hazifunguki Mkuu
Tafadhali hebu rudia tena na bila shaka nambari yako nimeichukua na ntakuseach hewani muda wowote! Asante sana!!!
Picha naona zimezuiliwa zisionekane na moderator nadhani.