Ufugaji wa Kware kwa sasa umekuwa wenye tija kubwa hasa kutokana na kware mwenyewe pamoja na mayai yake kutumika kama dawa kwa watoto na wazee. Kutokana na matumizi hayo, mahitaji ya kware na mayai yake yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku. Kwakuwa mahitaji ni makubwa kuliko uzalishaji wake, umefanya bei ya mayai na kware kuwa kubwa. Kwa sasa Bei ya kware inakwenda hadi tsh 30000/= wakati bei ya yai moja ni shilingi 1000/= kwa hiyo ukiwa na tray moja utaliuza kwa shilingi elfu thelathini.
Utunzaji wa Kware kimsingi hawana tofauti na utunzaji wa kuku. Hata kwenye upande wa chakula, ambacho kware anakula ni kama kile ambacho kuku anakula. Kitu muhimu cha kuzingatia ni kwamba kifaranga wa kware haitaji maji hata kidogo. Kifaranga wa kware akiloa maji unampoteza mara moja.
View attachment 219415 View attachment 219417 View attachment 219418 View attachment 219419 View attachment 219420 View attachment 219421
Bei ya kifaranga mmoja wa kware wa siku moja ni tsh 2700, wa wiki moja ni tsh 3800, wa wiki 2 ni tsh 10000/= Mayai ya kware tray moja kwa bei jumla tunauza elfu 18,000/=