mkulimamiwa
JF-Expert Member
- Mar 4, 2025
- 2,591
- 5,315
Salaaamu Wanabodi....!
Ngoja tutete kidogo, imma kwa Rais wetu ajaye ama vyovyote iwavyo
Tangu nimezaliwa hadi leo, nimebahatika kumuona tu kwa kipindi kifupi sana Baba wa taifa hili Mwl Julius Kamabarage Nyerere na siyo kuishi kwenye utawala wake
Ila nasikia huyu baba alikuwa na misimamo isiyoyumba hasa linapokuja suala la Nchi yake Tanzania na Africa kwa ujumla pamoja na uvunjaji wa katiba yetu licha kwamba ni mbovu, ila alisimama kidete kukemea na kuonya juu ya hayo
Ukiondoa huyo, pia miaka ya hivi karibuni, mtu mwingine ambaye nimebahatika kuuishi utawala wake akiwa Rais wa nchi na ambapo naye alikuwa na misimamo mikali, ni huyu aliyejulikana saaana mpaka kwa watoto wadoogo, Ndugu John Pombe Magufuli, Rais wa awamu hii inayoishiria na ambapo yeye aliishia njiani kwa Muumba wake kuamua kumchukua
Yeye ndo naweza kusema kwamba, siyo tu niliambiwa, bali nimeyaishi matendo yake, JPM alikuwa akisema, barabara itapita Ubungo na itanyooshwa pasina kupindishwa hata kama kuna ofisi za serikali, lazima zivunjwe barabara ipite na hata kukiwepo nyumba yake mwenyewe
Ilikuwa akisema jambo, wengine wenu hata msipounga mkono litafanyika tu ilimradi lina manufaa anayoona yeye
Kwa Marais wengine siwezi kusema sana maana hawakuwa na misimamo mikali kama ya hao wawili
Tukirudi sasa kwa huyu mwanachadema na mtu mwenye damu ya upinzani bwana Tundu Lissu
Unadhani ni kwa nini anamisimamo mikali kiasi hiko?
Unadhani misimamo ya bwana Lissu inamanufaa kwenye Taifa letu?
Mtu ambaye yupo tayari kufia jela na siyo kujikomba na kuwaangukia watawala kama ambavyo wengine wanafanya/wamefanya kina Mbowe, kina Jobu Ndugai na wenginewe
Mtu ambaye anaamini kwenye sheria na siyo desturi n.k
Unadhani huyu ndiye mtu sahihi?
Unadhani Taifa linahitaji mtu wa kaliba yake?
Unamaoni gani mwana JF mwenzangu